Tanzania yaziburuza Kenya na Uganda katika kilimo cha umwagiliaji, yazilisha mchele mara sita zaidi ya Kenya

Tanzania yaziburuza Kenya na Uganda katika kilimo cha umwagiliaji, yazilisha mchele mara sita zaidi ya Kenya

joto la jiwe

JF-Expert Member
Joined
Sep 4, 2017
Posts
26,117
Reaction score
46,617
TANZANIA imetajwa kuwa mzalishaji mkubwa wa mazao ya nafaka katika ukanda wa Afrika Mashariki, huku pia ikitajwa kuwa na fursa kubwa ya kutawala soko la Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika(SADC) kwa kutumia fursa za kilimo cha umwagiliaji.

Mfano umetolewa kwenye zao la mpunga, ambalo kwa sasa uzalishaji wake nchini umefikia tani milioni 2.1, wakati nchi za Kenya, Uganda uzalishaji wa zao hilo ni kati ya tani 100,000 na 200,000 tu.

Akizungumzia fursa hiyo kwa Tanzania wakati wa Maonesho ya Kilimo, Ufugaji na Uvuvi yaliyofanyika kitaifa mkoani Simiyu mapema mwezi huu, Mkuu wa Kitengo cha Ukaguzi na Udhibiti Ubora wa Tume ya Taifa ya Umwagiliaji (NIRC), Daniel Manase, alisema maboresho kwenye sekta ya kilimo cha umwagiliaji ndiyo yaliyoleta manufaa hayo.

Alisema baada ya kuundwa NIRC na kuanza kutekeleleza majukumu yake rasmi mwaka 2015, eneo linalomwagiliwa nchini limeongezeka kutoka hekta 461,333 mwaka 2015, hadi kufika hekta 694,715 mwaka huu.

Aidha, alisema skimu za umwagiliaji 2,555 zimesambaa nchi nzimam hivyo kutoa fursa kwa Tanzania kufanya vizuri zaidi kwenye kilimo hicho, huku fursa ya kuteka soko la EAC, SADC na Afrika kwa ujumla ikiwa kubwa endapo mkazo zaidi utawekwa kwenye kilimo hicho.

Akizungumzia kilimo cha umwagiliaji kwa nchi za Afrika Mashariki, Manase alisema Tanzania ikilinganishwa na mataifa mengine, ina fursa kubwa ya kuwa mzalishaji mkubwa wa mazao ya nafaka katika Afrika kupitia kilimo cha umwagiliaji.

Alisema kwa mwaka, Tanzania hupata mvua ya wastani wa milimita 950, huku eneo linalolimwa mpunga kwa sasa likiwa hekta milioni 1.23 na eneo lililoendelezwa kwa umwagiliaji likiwa hekta 694,715.

Alisema uzalishaji wa mpunga nchini kwa sasa ni tani milioni 2.01 kwa mwaka, huku tija ikiwa ni tani 1.5 hadi 8.1 kwa hekta.

Alisema Tanzania ina eneo la hekta milioni 29.4zinazofaa kwa kilimo cha umwagiliaji na kati ya hizo, milioni 2.3zina uwezekano mkubwa wa kumwagiliwa, milioni 4.8zina uwezekano wa kati na milioni 22.3zina uwezekano mdogo wa kumwagiliwa.

Manase alisema hivi sasa Tanzania inajitosheleza kwa chakula na ina akiba tani milioni 2.79, ambazo zimetokana na mikakati ya nchi kwenye kilimo kwa kutumia pembejeo bora, kuimarisha mifumo ya kilimo na kutoa fursa ya mikopo ya kilimo bila riba.

Kwa upande wa Kenya, hupata mvua ya wastani wa milimita 500 hadi 2,000 kwa mwaka, huku eneo linalomwagiliwa likiwa hekta 125,000 na jumla ya eneo linalofaa kwa umwagiliaji ni hekta 1.3 na uzalishaji wa mpungua kwa sasa ni wastani wa tani 150,000, huku tija ya uzalishaji wa mpunga kwa sasa ni tani 1.1 hadi 5.2 kwa hekta.

Nchini Uganda, uzalishaji wa mpunga umetajwa kuwa wastani wa tani 215,000, wakati mahitaji ya nafaka hiyo ni tani zaidi ya 230,000, hivyo kuwa na mahitaji ya kuagiza mchele kutoka nje ya nchi hiyo.

Hata hivyo, eneo linalofaa kwa umwagiliaji kwa ujumla nchini Uganda ni hekta milioni 3.03, lakini lililoendelezwa kwa kilimo hicho ni dogo ikilinganishwa na ukubwa uliopo.

Kwa mujibu wa taarifa kutoka Shirika la Chakula Duniani (FAO), kilimo cha umwagiliaji kimechangia kuongeza tija ya uzalishaji na uzalishaji wa mazao mbali mbali katika miongo ya karibuni barani Afrika na na kutaka mkazo uwekwe na nchi hizo kukiendeleza kwa sababu ndio eneo bora zaidi lenye tija ya kweli.

Mafanikio mengini ya kilimo cha umwagiliaji ni kupitia mazao ya mbogamboga, ambapo Meneja Mazingira ya Biashara wa Taasisi Binafsi inayoundwa na wadau wa mnyororo wa thamani wa kilimo cha mbogamboga, matunda na viungo (Taha), Kelvin Remen, amesema kina tija iwapo wakulima wataweka mkazo.

Tanzania yawa kinara uzalishaji nafaka EAC

========

MY TAKE:
Hivi kweli kuna mkenya ambaye bado anadhani Kenya inaweza kushindana na Tanzania?
 
Mkuu unaposema skimu 2555 zimeongezeka je unazungumzia skimu za mfano wa kapunga irrigation au wami dumila skimu naomba ufafanuzi?
 
Mfano umetolewa kwenye zao la mpunga, ambalo kwa sasa uzalishaji wake nchini umefikia tani milioni 2.1, wakati nchi za Kenya, Uganda uzalishaji wa zao hilo ni kati ya tani 100,000 na 200,000 tu.

WaKenya watakuja na mahesabu ya magunia milioni 98 yanazalishwa Kenya, ili kulinganisha na tani milioni 2.1 za Tanzania.

Halafu watabishana kwa mzania huo kuwa wanazalisha zaidi kuliko nchi yoyote ukanda wa Afrika ya Mashariki.

Ngoja tuwasubiri waje watoe idadi ya magunia !
 
Mavuno ni meng katika nchi ya maziwa na asali Tanzania.
 
Kwa ukubwa, na rutuba ya ardhi yetu tulitakiwa tuongoze kwa kila kitu sio mchele tuu, mazao menhi muhimu tungezalishqa kwa wingi hata hizo tani million za mchele ni ndogo, tuongezee juhudi.
 
Kwa ukubwa, na rutuba ya ardhi yetu tulitakiwa tuongoze kwa kila kitu sio mchele tuu, mazao menhi muhimu tungezalishqa kwa wingi hata hizo tani million za mchele ni ndogo, tuongezee juhudi.
Kaka hiki tunachozungumza ni kilimo cha kumwagilia ambacho hakitegemei rutuba ya ardhi, kumbuka Egypt ndiyo inayoongoza Africa kwa uzalishaji wa mpunga wakati ile nchi ni jangwa ila kilimo cha umwagiliaji ndio kimewaokoa, Israel hivyo hivyo. Hapa sababu ya kutozalisha kwa kusingizia ardhi haipo.
 
Kaka hiki tunachozungumza ni kilimo cha kumwagilia ambacho hakitegemei rutuba ya ardhi, kumbuka Egypt ndiyo inayoongoza Africa kwa uzalishaji wa mpunga wakati ile nchi ni jangwa ila kilimo cha umwagiliaji ndio kimewaokoa, Israel hivyo hivyo. Hapa sababu ya kutozalisha kwa kusingizia ardhi haipo.
Okay. Nimekupata mkuu
 
Hayo maziwa mengi mnayo na kupelekea muwe na maji mengi,eneo la ardhi kubwa mnayo sioni cha ajabu hapa,mlitakiwa mlime hata mara 100 zaidi ya hayo.
 
Hayo maziwa mengi mnayo na kupelekea muwe na maji mengi,eneo la ardhi kubwa mnayo sioni cha ajabu hapa,mlitakiwa mlime hata mara 100 zaidi ya hayo.
Muhimu mkubali kwamba sisi ndio baba lao mitaa hii, ninyi si mnasifia GDP kubwa, kwanini msigeuza Turkana ikawa ni eneo la kilimo kama ilivyofanya Israel?, au ni GDP ya kwenye makaratasi lakini hata Galana Kulalu limeshindikana?. Hamuoni aibu nchi yenye GDP kubwa kuwa hekta 150,000 pekee za irrigation?, hii ni aibu sana.
 
Back
Top Bottom