Tanzania yazindua teknolojia ya kipekee ya DNA

Mkalukungone Mwamba

JF-Expert Member
Joined
Aug 29, 2022
Posts
3,141
Reaction score
7,205
Mamlaka ya Afya ya Mimea na Viuatilifu Tanzania (TPHPA) imezindua teknolojia mpya ya kisasa inayotumia kipimo cha DNA kubaini magonjwa ya wanyama na binadamu, visumbufu vya mazao, na kutoa majibu ya kitaalamu kwa uchambuzi wa kiuchunguzi (Forensic Analysis).

Akizungumza na wanahabari jijini Dodoma leo, Agosti 6, 2025, katika Viwanja vya Maonesho ya Wakulima, Wafugaji na Wavuvi maarufu kama Nanenane, Profesa Joseph Ndunguru amesema teknolojia hiyo, ambayo kwa sasa katika Sekta ya Kilimo inapatikana Tanzania pekee duniani, itasaidia kubaini magonjwa ya mimea na wadudu wanaoshambulia mimea, hivyo kumwezesha mkulima kutumia kiuatilifu sahihi.

“ Na niwaambie tu kwamba sisi watanzania ndio wakwanza duniani kukiingiza hicho kifaa kwenye Sekta ya Kilimo kwahiyo mjue hilo, ni teknolojia ya juu sana” Amesisitiza Prof. Ndunguru

Ameongeza kuwa kifaa hicho kinatoa majibu ndani ya dakika 20, hivyo mkulima hahitaji kupeleka sampuli maabara, bali anaweza kutumia kifaa hicho papo hapo shambani. Kwa sasa, TPHPA ina vifaa 20 vya aina hiyo ambavyo vitagawanywa katika kanda zote za nchi ili kutoa huduma kwenye mikoa yote ya Tanzania.

Aidha, amesema teknolojia hiyo itasaidia pia katika usafirishaji wa mazao ya biashara kwenda nje ya nchi kwa kuwezesha kubaini vinasaba vya mazao. Hii itasaidia kukidhi vigezo vya masoko ya kimataifa na kuzuia udanganyifu wa bidhaa zisizo za nchini kuuzwa kama za Tanzania. “Mfanyabiashara asiye mwaminifu akichukua mchele wa India na kusema ni wa Tanzania, kifaa hiki kitaonyesha moja kwa moja kuwa huo ni wa India na si wa Mbeya,” alisema Profesa Ndunguru.

Kifaa hicho pia kina uwezo wa kubaini magugu vamizi, kuchunguza ubora wa mbegu, kufanya uchambuzi wa kiuchunguzi, kubaini magonjwa ya mifugo, wanyama pori na hata binadamu. Pia kinaweza kupima maji na kubaini kama yanafaa kwa matumizi ya binadamu, sambamba na kusaidia kuandaa kanzidata ya vinasaba vya wanyama pori ili kudhibiti ujangili.

snapins-ai_3693389367519628934.jpg
snapins-ai_3693389367527868752.jpg
 
View attachment 3434285View attachment 3434286
Jambo jema!
 
Nimeishia hapa """teknolojia ya juu sana” Amesisitiza Prof. Ndunguru"""

Hii ni copy and paste kutoka huko Duniani. Janja janja na utapeli wa taarifa zilizo bayana huko mtandaoni ni Ulimbukeni.

Prof. Ndunguru Ajitathmini!
 
Back
Top Bottom