FredySenior
New Member
- May 25, 2024
- 2
- 3
TANZANIA YENYE AJIRA LUKUKI INAWEZEKANA Likifanyika Jambo Hili.
Twende Moja Kwa Moja Kwenye Point, Sekta Binafsi Ni Moja Ya Sekta Muhimu sana katika kuzalisha Ajira.
Sitaki kuongelea Mazingira Yaboreshwe kuruhusu Uwepo wa Sekta Binafsi nyingi,
Nachotaka Kushauri Mimi ni hiki hapa.. SERIKALI IFANYE UWEKEZAJI MAALUMU WA KUMILIKI HISA katika kampuni, viwanda au biashara za vijana wa kitanzania.
KIVIPI? Iko hivi, Hapa Tanzania Vijana ni wengi wanaojaribu kuanzisha Kampuni, Viwanda Hata Biashara Kubwa Lakini Wengi wao wanafeli, kwanini wanafeli?
Baadhi ya Sababu ni Hizi Hapa;
1: Pesa Za Uendeshaji
2: Maarifa ya Uongozi na uendeshaji
3: Elimu ya udhibiti fedha
4: Mazingira kutokua rafiki hasa kutoka kwenye mamlaka
NINI KIFANYIKE?
iko hivi, Serikali Itengeneze kitu kama WIZARA MAALUMU YA UWEKEZAJI, ambapo itakua na jukumu la kufatilia na kutafuta hizi kampuni, viwanda au biashara za mawazo bunifu zinazoanzishwa na vijana kisha INAWEKEZA kwenye hizi Kampuni, viwanda, mawazo bunifu hata biashara za vijana wa kitanzania kwa KUCHUKUA IDADI FULANI YA SHARES
yaani huu uwekezaji usiwe MSAADA (kwasababu mambo ya upigaji yatakua mengi) bali uwe ni UWEKEZAJI wenye TIJA ambapo SERIKALI kupitia wizara hiyo maalumu na wao watakua WAMILIKI wa hiyo kampuni kwa kumiliki HISA kadhaa za kampuni, kiwanda au biashara ya huyo kijana wa kitanzania, lakini Kampuni, kiwanda au biashara itaendelea kumilikiwa kwa asilimia kubwa na huyo kijana/vijana
NASHAURI mchakato wa kupata sehemu hizi za kuwekeza uwe wa wazi ili kuondoa upigaji, inaweza kufanyika kama SHINDANO, ambapo vijana watawasilisha StartUp zao au biashara zao walizoanza kuzifanya, kisha serikali kupitia wataalamu wao itafanya tasmini na kuamua kuwekeza. (Mfano ile Project/Tv program ya SHARK TANK wanavyofanya kupata sehemu za kuwekeza)
FAIDA YA LENGO HILI ni kwamba, kwasababu Serikali itakua ni sehemu ya Wamiliki itaweza kufahamu muenendo wa Kampuni husika kupitia ripoti za mara kwa mara, ambazo huwa zinatumwa kwa wawekezaji wote. Jambo ambalo litafanya ukuaji madhubuti wa kampuni, kiwanda au biashara husika.
ILI KUJIDHATITI:
serikali kupitia Wizara hii Maalumu ni vyema ikawa na wataalamu wa maswala yafuatayo ambayo mimi binafsi kama Mkurugenzi wa kikampuni changu kidogo nimegundua yanachangia kufeli kwa StartUp nyingi.
1: wataalamu wa maswala ya Fedha
2: wataalamu wa maswala ya mifumo ya technolojia
3: wataalamu wa maswala ya uongozi na sheria
Ambapo watu hawa watakua wanasambazwa kwenye Kila Sehemu ambapo Serikali inanunua hisa, watakua kama wafanyakazi ambao watalinda maslahi ya serikali.
KWA DHATI kabisa Naamini Jambo hili likifanyika Serikali inaweza kuzalisha AJIRA nyingi sana kupitia AINA HII YA UWEKEZAJI.
Mfano: serikali ikitenga BILIONI 10 kuwekeza Tsh MILIONI 50 kwa kila uwekezaji, hapa itakua imewekeza kwa viwanda, kampuni au biashara takribani 200, endapo ndani ya miaka 10 kila sehemu walipowekeza watafanikiwa kuajiri Vijana 50 maana yake vijana ELFU 10 watakua wameajiriwa.
Na endapo sehemu zote hizo walizowekeza zikianza kutengeneza Faida ndani ya miaka kumi, tunategemea miaka 10 tena ijayo serikali itakua na uwezo wa kuwekeza Mara Mbili ya ilivyofanya mwanzo. Kwahiyo itaweza kutengeneza tena ajira za moja kwa moja zaidi ya ELFU 20
Tanzania Tuitakayo Inawezekana.
ASANTE, NAWASILISHA WAZO LANGU.

Upvote
2