Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Bora humu tunaingia kwa id na majina bandia. Kama tungekuwa tunatumia picha na majina halisia basi tungedharauliana waziwazi. Sikuelewi hata chembe
Hii ni taarifa toka kwa mshirika mnafiki.
BD wanajua hakika namna serikali hii na iliyopita ilivyochezea na inavyoendelea kuchezea rasilimali za taifa na kufukarisha umma kwa manufaa ya kikundi kidogo cha watu 'wanaohesabika'.
Ukiamua kuzifuatilia takwimu hizi bila kujihoji, maendeleo kwako utayasikia na kuyapigia makofi toka kwa jirani yako
Ndiyo, wameweza kuingia na kuchota mali ya taifa jinsi watakavyo, wananchi wakifukuzwa kwenye maeneo yao kama nguruwe pori, huku watetezi wao wakikenua meno bila msaada wowote. Ndiyo maana taarifa zao ni za kuwafurahisha watawala wetu waendelee kukenua menu, nchi na wananchi wake wakiteketea kwa njaa.
Nyama ya mifupa inauzwa 5,000/=
Mchele 2,500/=
Sukari 2,500/=
Unga 800/=
Mafuta ya taa vijijini 2,500/= - 3000/=
Dagaa 5000/=
Mchicha fungu 1000/=
Labda ni kwa sababu serikali imeachana na matumizi ya fedha yetu ya shilingi kwa matumizi yote ya ndani na kutumia pesa yao ya dola?
Serikali imeshidwa kabisa kulipia huduma zake kama mishahara, elimu, madawa nk. huku miradi yote ya maendeleo inayofadhiliwa na serikali ikiwa imesimama. Moto wake utakapolipuka hiyo midomo iliyofungwa hakuna mamlaka itakayoweza kuinyamazisha.
Mercy acha ulaghai wako kwa Watanzania na ripoti yako mbovu mbovu.
Great, kwanini tusiondoe kikomo cha uongozi ili aendelee kufanya vizuri?
hii stori imepikwa
Acha uongo mazeei! Makatambuga yalianza kuvaliwa miaka ya 80's baada ya kuambiwa tufunge mikanda kwa miezi 18. Kabla ya hapo mambo yalikuwa poa sana!
Mama Clinton pia alikuja kuipa shavu Symbion. Hakuna mtu mwenye uelewa wa macro-economics hapa duniani anayezingatia maoni ya WB na IMF kama kigezo/mkakati wa maendeleo. Hizo taasisi zipo kutengeneza mazingira mazuri kwa matajiri binafsi hususan wa US na ulaya kujichumia bila udhibiti. Wachina na wajanja wengine walishasoma mikakati hiyo zamani sana ndio maana wanaheshimika kikweli. Hata kelele kuhusu "haki za binadamu" siku hizi zinatolewa kiganjani!
Kwa WB na IMF, Tanzania ni uwani (backyard) au banana republic nyingine ambayo imeachia kila upenyo kwa "wazito" kujinafasi kiuchumi kwa raha zao. Kwa nini wasiimwagie mvua ya misifa! Ni aibu mtu kufurahia kusifiwa na taasisi hizo. Jana niliwasikia wakidai eti TZ yaweza kufikia nchi za uchumi wa kati mapema almuradi idhibiti "ufisadi" unaoanza kuwa tishio. Ni kama vile waliona haya kidogo kutoingiza suala hilo lililopo nje-nje hivi sasa. Kufikia uchumi wa kati? Are these guys comedians?
MD, siasa gani hapo umeona kutoka kwa world bank? Si wamesema tuwekeze kwenye elimu na job creation ili tu bounce back. hebu acheni kuweka siasa kwenye kila kitu.
MD, siasa gani hapo umeona kutoka kwa world bank? Si wamesema tuwekeze kwenye elimu na job creation ili tu bounce back. hebu acheni kuweka siasa kwenye kila kitu.
Mkuu soma btn the lines utanielewa.
Kusema tu uchumi utakuwa kwa 7% 'IF' uchumi wa ulaya au US utakua stable, au tuongeze electricity generation, au job creation au etc HAITOSHI!
Kwanza kwa upande wa power generation si unaona umeme wa mafuta unavyotudidimiza?
Cha maana ni lazima hawa magamba wakubali kutengeneza 'National Strategies' ambazo watazisimamia ipasavyo, hapa siongelei Ilani ya chama chao kilichokosa mwelekeo.
Nchi inaitaji Strategic repositioning.
Hawa World Bank, wanachokifanya ni kuteendeleza propaganda zao za western, afu kwa dizaini ya prezident tulie nae anapenda sana kusikiliza statistical views kama hizo, na wao WB wanalijua hilo.
Mkuu wake up!