SoC04 Tanzania Yenye Wananchi Walio Huru Kiuchumi

SoC04 Tanzania Yenye Wananchi Walio Huru Kiuchumi

Tanzania Tuitakayo competition threads

concious mind

JF-Expert Member
Joined
Jun 27, 2012
Posts
1,003
Reaction score
617
JIWEKEE AKIBA UWE HURU KIUCHUMI

Katika hali ya kawaida watanzania wengi hatuna tabia ya kuweka akiba. Hii imetokana na mazoea ya kawaida ya kuishi kutokana na kipato tunachopata. Tabia hii imejengeka kwa watu wa kipato cha chini hadi wale wenye kipato kikubwa, watu wasio na kipato rasmi hadi wale wenye kipato rasmi.

Kuna faida nyingi za kujiwekea akiba hususani zile za muda mrefu. Faida hizi ni kwa mtu mmoja, jamii na taifa. Kumekuwa na mawazo kwamba ukipata hela nyingi ndio unaweza kutunza akiba. Wazo hili sio sahihi kwa sababu katika wakati wowote tunatakiwa kutunza/akiba. Maana ukisubiri uwe na hela nyingi ndio utunze akiba unaweza pata changamoto ukajikuta hauna hata akiba ya kuweza kukusaidia. Akiba zipo za aina nyingi ila akiba ya muda mrefu ndio hasa ambayo kila mmoja anatakiwa kuwa nayo.

Kuna akiba tatu za muhimu kuwa nazo, akiba ya kwanza ni akiba maalumu, hii ni akiba kwa ajiri ya kufanya jambo fulani. Katika akiba maalumu watu wengi tumejitahidi na huwa tunafanya mfano akiba kwa ajiri ya kujenga, akiba kwa ajiri ya kununua gari au kulipa ada za watoto.

Akiba ya dharura akiba hii ni namba mbili kwa umuhimu kwani ndio msingi wa mtu kuendelea hasa pale unapopata majanga yanayolazimisha kuanza upya kifedha. Kimsingi akiba hii inatakiwa iwe ni mara sita ya matumizi yako ya mwezi. Kwa mfano kwa mwezi matumizi yako ni milioni mbili (2,000,000/=) basi akiba hii inatakiwa kuwa ni milioni kumi na mbili (12,000,000/=). Hii itakusaidia kuendelea kuishi bila changamoto pale itakapotokea tumekwama kabisa kifedha.

Akiba ya tatu ni akiba ya muda mrefu, akiba ya kustaafu au waweza kuiita akiba ya uzeeni. Akiba hii ndio hasa lengo la andiko hili. Kimsingi tunapozeeka inafikia hatua hatuwezi tena kufanya kazi za kujiingizia kipato. Hii inaweza kuwa sababu ya umri au magonjwa ya uzeeni. Basi ni wakati huo kama ulijiwekea akiba itaweza kukusaidia kumudu matumizi yako ya kila siku na kuepuka kuwa tegemezi. Ni katika wakati huu watu wengi wanapatwa na magonjwa ya moyo sababu ya kupigwa na maisha na wengine wamegeuka tegemezi kwa watoto na omba omba kwa jamii inayowazunguka.

Kuweka akiba ni rahisi sana lakini pia ni ngumu sana. Hakuna kitu kigumu au kirahisi kama kinavyoonekana. Alisema mwandishi John C Maxwel. Ugumu na urahisi wa kuweka akiba itategemea na mipango yako unayojiwekea mwenyewe. Kimsingi kila mtu anauwezo wa kujinyima na kuweka akiba sehemu ya kumi ya pato lake. Mfano mtu anapata laki moja na nusu kwa mwezi (150,000/=) huyu mtu anauwezo wa kusave elfu kumi na tano kwa mwezi(15,000/=). Kwa mtu anayeingiza milioni moja(1,000,000/=) kwa mwezi anauwezo wa kusave laki moja(100,000/=) kwa mwezi.

Tunapoongelea kuweka akiba tunaongelea asilimia ya pato lako na sio kiasi fulani cha pesa, ikiwa unaingiza pesa kidogo unatakiwa utunze hela kidogo na kama unaingiza pesa nyingi basi unatakiwa kutunza hela nyingi.

Je ni kiasi gani mtu anaweza kuweka akiba? Wengi tunajiuliza swali hili lakini ni wachache wamefanikiwa kupata jibu la kuridhisha. Kimsingi usiweke lengo kubwa sana kuliko kipato chako lakini pia usiweke lengo dogo sana. Ukijiwekea lengo/kiasi kikubwa sana utashindwa kuweka na hatimaye itakukatisha tama. Ukijiwekea lengo dogo sana akiba hiyo haitakusaidia maana mwisho wa siku utakuwa na akiba ndogo sana. Mwandishi Napolean Hill katika kitabu chake cha law of success ameshauri kutumia mtiliko ufuatao ili kujua uweze kusave kiwango gani kwa mwezi kutoka katika pato lako

Kiwango cha akiba……………………..…….................................. 20%

Mahitaji ya lazima – Chakula, nguo na malazi.. 50%

Elimu …………………………………..…......................................................... 10%

Kujiburudisha/Tafrija…………….................................……………. 10%

Bima ya maisha……….……….....................................……………….. 10%

100%

Mali bila daftari hupotea bila habari, ikiwa hatujui tunatumia kiasi gani kwa mwezi kwenye kitu gani hatuwezi kujua kujua tunatumia pesa vibaya. Kupitia andiko hili ninahamasisha kila mmoja kuweka akiba japo asilimia kumi tu ya kile anachokiingiza.

Ukiweka pesa kidogo kidogo bila kuitoa kwa mda mrefu basi unapata faida kubwa, mifuko/akaunti nyingi zinatoa gawio la asilimia 10 hadi 15 kwa mwaka kwa akiba za muda mrefu.

Watu wengi wanafahamu haya na hawaweki akiba kwa makusudi au kwa kushindwa kujua waiweke wapi akiba yao. Kama upo kwenye kundi la wasioweka akiba kwa sababu umeamua tu nakushauri ujitafakari tena na tena kwani mara nyingi majanga huja bila hodi. Je umeshawahi kujiuliza ikitokea leo hauwezi kuingiza pesa utaweza kuishi maisha ya kiwango hicho unachoishi kwa muda gani? Je miezi sita itafika kabla haujaanza kupiga watu vizinga?

Kwa kundi ambalo hatujui tuwekeze wapi basi napendekeze mifuko miwili 1 Hati fungani (Treasure bonds) 2. UTT. Napendekeza huku kwa maana nina uzoefu nayo na watu waliowekeza huku sijasikia kama kuna changamoto.

Ikiwa utawekeza pesa kwa muda mrefu basi utapata faida na pesa yako itaendele kuongezeka kidogo kidogo kadiri muda unavyoenda. Kwa maneno mengine kiasi chochote utakachoweka baada ya miaka ishirini na tano (25) tegemea pesa yako kujizalisha mara mia moja (100). kwa mfano ukiweka milioni moja kwa kila mwaka(1,000,000) baada ya miaka ishirini na tano (25) utakuwa na jumla ya milioni mia moja (100,000.000). Hii inamaanisha ukiweka milioni moja (1,000,000) kwa mwaka baada ya miaka ishirini na tano (25) utatangeneza faida ya milioni sabini na tano (75,000,000) hapa ni kwa mahesabu ya gawio la asilimia kumi(10) kwa kila mwaka.hii inawezekana kama tu hautatoa chochote katika akiba yako hii na kila gawio unalopata utaliongezea kwenye akiba yako.

Jedwali hapa chini ni mfano wa ongezeko ukiwekeza katika mfuko utakaokupa gawio la asilimia kumi (10%)



JIKOMBOE KIUCHUMI
MIAKA WEKA GAWIO JUMLA
11,000,000o1,000,000
21,000,000100,0002,100,000
31,000,000210,0003,310,000
41,000,000331,0004,641,000
51,000,000464,1006,105,100
61,000,000610,5107,715,610
71,000,000771,5619,487,171
81,000,000948,71711,435,888
91,000,0001,143,58913,579,477
10 1,000,000 1,357,948 15,937,425
111,000,0001,593,74218,531,167
121,000,0001,853,11721,384,284
131,000,0002,138,42824,522,712
141,000,0002,452,27127,974,983
15 1,000,000 2,797,498 31,772,482
161,000,0003,177,24835,949,730
171,000,0003,594,97340,544,703
181,000,0004,054,47045,599,173
191,000,0004,559,91751,159,090
20 1,000,000 5,115,909 57,274,999
211,000,0005,727,50064,002,499
221,000,0006,400,25071,402,749
231,000,0007,140,27579,543,024
241,000,0007,954,30288,497,327
25 1,000,000 8,849,733 98,347,059
Imeandaliwa na Concious Mind


Ukifuatilia vizuri miaka kumi na tano ya kwanza pesa inaongezeka kidogo kidogo sana ila baada hapo inaongezeka kwa haraka zaidi. Unaweza kuweka akiba anza sasa.
 
Upvote 6
Changamoto kubwa ni kuwa watu wengi hawataki kutunza akiba kidogo kidogo wakiona wanachelewa kufikia malengo yao. Lakini je ni afadhali kuchelewa kufika au kutofikia kabisa uhuru wa kiuchumi?
 
Uzi mzuri,Hizo Government bond unawekezaje
Kuna hatua tatu nyepesi za kuzifuata
1.Unafungua account katika benki zilizoingia ubia na BOT, Mfano Bank Of Africa, CRDB NK
2. Unawajulisha hiyo benki kuwa upo interested kununua bonds. Hivyo watakufungulia account BOT.
3. Unakuwa unafuatilia calendar za minada ya Treasury Bonds na kuandika barua kwenda benki uliyofungulia account kununua bonds za tarehe husika.
 
Back
Top Bottom