Tanzanian actor Steven Kanumba reported dead

tafadhari wenye picha yake jamani wengine hatumjui, Coz utadhani rais kafi.
 
Kanumba wiki iliyopita katika kipindi cha Take One kinachorushwa hewani kupitia Clouds TV alimtolea uvivu baba yake, Mzee Kusekwa akidai amechangia katika mateso yake aliyoyapata utotoni.


Kifo cha msanii steven Kanumba kimesababishwa na radhi ya baba yake mzazi

Wote wawili hapo kwenye RED mnatakiwa mkapimwe akili zenu. Hakuna sentensi au hata nukta katika historia ya binadamu inayoonyesha kwamba mzazi ana haki ya kumfanyia ukatili mwanae!

Kanisa Katroliki linapogundua mzazi kamfanyia ukatili mwanae kwa kumuua kwa njia ya abortion basi hata kumzika hatumziki kikanisa.

Mnaotuletea ujinga huu kwenye RED nahisi ni wavivu wa kuheshimu haki za watoto wenu na mnadhani kwa kufanya hivyo tutawatetea hapa jamvini.

Mbona Master Taji Liundi alisimulia magazetini jinsi mama yake mzazi alivyofanikiwa kuwaua ndugu zake lakini yeye aliokoka kimaajabu na hadi leo anaishi na tunamsikia redioni.

Ushamba wenu hauna mtetezi. Kuweni na adabu kwa haki za binadamu na haki na mtoto. Binafsi mimi mama yangu mzazi alichonifanyia kama hatakuja kujisumbua kuniomba walau kutamka neno "samahani" basi hata ulimwengu mzima upige kelele haimsaidii kitu na tutakutana kaburini.

Unapochangia hili, haisaidii kubadili kama ambavyo kiburi cha Baba Kanumba hakikumsaidia na sasa Kanumba watakutana na baba yake mbele ya Hakimu Mungu baada wote kuondoka hapa duniani.

Hongera Kanumba kwa kusimamia na kueleza ukweli ulivyonyanyasika, tutakutana ahera.
 
Reactions: 3D.
Wasanii watazika wasanii wenzao na Wasomi watazika wasomi wenzao..............

Wewe unaona cha Kanumba lakini kuna wengine wanaona cha Prof.
 
Mwana usijidai fan wa movie za mbele bsd it seemz hata unaowafagilia wa mbele wapata stori za kanumba. So acha mashauzi
 



Kama baba alimtelekeza Kanumba alikuwa na Haki kusema hisia zake,wewe unajua athari ambazo mtoto anaishi nazo kwa kutelekezwa na Baba yake? Si jambo jepesi,huyo baba yake Kanumba alitakiwa amwombe radhi mwanae kwa kumtelekeza kama ni mwenye Akili Timamu na Mwenye Hofu ya Mungu!!

Neno la Mungu linatutaka Watoto tuwaheshimu wazazi wetu ili tupate HERI na MIAKA mingi lakini ni Biblia hiyo hiyo inawaonya Wazazi KUTOKUWACHOKOZA watoto wao!!

Baba anapomtelekeza Mtoto,halafu mtoto akikuwa akisema kama ulimtelekeza unasemaje kwamba anakuvunjia Heshima? Utakuwa Mwehu na Tabia ya Wanaume Waovu ambao Ukimbia kulea watoto halafu akikuwa anajifanya kuwa karibu naye kuliko hata mama ambaye alimlea mwana kwa dhiki nyingi!!
Imeandikwa "Laana Isiyo na Sababu Haimpigi mtu",Kuhusu watu wanaotelekeza watoto wao Mungu anasema hivi "Yeye ni MBAYA asiyewahudumia Watu wa Nyumbani mwake kuliko asiye Amini"
Kwa maana hiyo basi,kama Kanumba amefariki ni kwa sababu zingine lakini siyo radhi ya huyo Mzee Hopeless and Irresponsible,kwa Mungu huyo ni MBAYA na atatoa Hesabu kwa nn alitelekeza Mwana!!

Kizee kama hicho hapo sasa kitakuwa kinawaza Mirathi tu maana hakina Uchungu,U cant Lose what u never had!!
 
mi maswala ya mziki na filamu, yamenipitia pembeni kabisa, cz nimekaa jela kamiaka 5 ndo nimetoka juz juz.
 
[Watu wanazungumzia msanii wa filamu we unaleta mambo ya juma nAture... Wa wapi wewe
 
Inategemea na watu wengi wapo kundi gani. Kwa wasomi kama mimi, kifo cha Prof kinakuwa na uzito kuliko cha msanii ambaye hana mchango wa karibu katika maisha yangu au kifo cha rais wa nchi nyingine. Kwa watu wa filamu na udaku udaku na usanii, kifo cha msanii kinakuwa na uzito kwao kuliko cha Prof, kwani kwao elimu haina maana. Kwa waMalawi waliopo Tanzania, kifo cha rais wao kina uzito kuliko msanii wa bongo na Prof wa bongo. Sasa kama utafiti wako upo sahihi na umeonyesha Kanumba kawafunika wengine, basi unatakiwa kugundua mara moja kuwa waTanzania wasomi walioshtushwa na kifo cha Prof ni wachache (na huo ndio ukweli, nchi hii ina wasomi wachache kuliko wajinga), na waMalawi waliopo nchini ni wachache kuliko waTanzania wanaopoteza muda kuangalia movies za Kanumba (na huo ndio ukweli, sitegemei kuwa na Wamalawi wengi nchini kuliko wasoma magazeti ya udaku yanayoandika wasanii kila siku). Kwa hiyo hii thread haiko valid, kwani ni kitu kinachotazamiwa kabisa. Lakini kukiwa na coincidence ya mazishi na iwapo kuna ulazima wa kuhudhuria mazishi, mimi nitahudhuria ya Prof (wengine hudhurieni ya mcheza filamu)
 
Mods tafadhali if u are serious delete hii thread inaivunjia heshima JF na members wengine!
Ki vipi mkuu? Hii topic ilianzishwa tarehe 2 March 2012, zaidi ya mwezi mmoja kabla ya Kanumba kufariki. Au sijaelewa concern yako?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…