Usiku wa kuamkia Ijumaa (Jana) niliota ndoto ya ajabu. Kwamba nilikuwa katika mji fulani mkubwa, lakini ghafla mawinguni upande wa magharibi nilikiona kikundi cha wasanii, walikuwa kama wa tano hivi. Wote wakiwa ndani ya suti nyeusi na mashati meupe na bulls' tie. Nilivyo waona ilikuwa kama vile "projector" ilikuwa mahali na kutumia mawindu kuwa kama 'screen'. Picha za wale wasanii zilikuwa ni aina ya pasipoti ila zilikuwa kubwa sana na nilimfahamu kiongozi wa kikundi kile aliyekuwa mbele na ukubwa wake wa pale mbele aliwaziba wengine wa nyuma. Huyu mtu alikuwa ni Steve. Basi sikujali.Lakini nikaenda mji mwingine mdogo, kule tena ile picha ikaibuka. Safari hii wale wasanii wakaimba sana mziki wakifurahi (ilikuwa kama move hivi). walipomaliza ile picha ikatoweka, na mimi nikasema vijana hawa wameanza usanii hivi karibuni lakini wamestawi sana.
Saa hivi wakati naangalia historia ya marehemu TBC, ile ndoto niliyokwisha isahau ika-flash kwenye kioo cha dirisha. Ndipo nimekumbuka ndoto hii nakuiweka hapa.