Tanzanian doctors oppose Kenya's plans to hire them

True that... When Kenya is Ranked the 157th most Corrupt Country in the world; Hata president Heshima zake aokote kwa choo....
 

 

Hata kama wameenda shule miaka kumi, hilo halina mantiki wala nini, Wakenya wasiokua na uwezo kule vijijini wanateseka, na pande zote mbili zinatunishiana misuli halafu nyie kazi kushabikia bila kufikiria kusudi mkwamishe gurudumu la taifa na kupata cha kutumia kulaumu mkiwa kwenye kampeni.

Binafsi ningependa madaktari wapewe maslahi yao, maana hata kwetu nyumbani nina watu wetu kwa familia ambao ni madaktari hivyo sio nyie wa upinzani tu mnaotaka madaktari kiunafiki, hata sisi wengine tunawapenda na tunataka walipwe vizuri maana ni ndugu zetu na tupo nao kwenye jamii. Lakini hata hivyo kwenye kila mgogoro lazima pawe na suluhisho sio kutunishiana misuli kila siku kwa miezi huku Wakenya tukiteseka eti kisa wamesoma miaka saba, kwani wengine tuna taaluma zetu pia.

Hao madaktari wakubali kufika kati na serikali ikubali kufika kati, wakutane na kusuluhisha, vinginevyo ipatikane suluhu nyingine hata kama ya kuwaleta madaktari kutokea ahera.
 
Before you work as a medical doctor in Kenya, you must be registered with the medical board of Kenya.
Hii story ya imported doctors can't work. So Tanzania better not get excited. Hapa lazima labda kuwe na special exemption.
Kasome hizo sheria vizuri. Mtu yeyote anaweza kufanya kazi sehemu yoyote katika field ya AFYA ila atapaswa kusajiliwa na taasisi husika na kuna taratibu atapaswa kuzifuata;

Atapewa "Temporary registration" then atatakiwa kufanya kazi chini ya uangalizi kwa kipindi maalumu (Usually 6 to 12 months, then anakuwa granted "Full registration."

Hata hapa Tanzania sheria hiyo ipo..!
 
Seriously, wangapi watz wanahudumu Kenya. For Commonwealth countries that may apply. But even with that exception, the country of origin must confirm that the said doctor is registered. So, having realized that any foreign doctor would have to be vetoed by the medical practioners and dentists board, who by the way are pro kmpdu. What makes you think even a single tz doctor would pass.
 
In Kenya you are either registered or not. Hanna temporary registration humu. And no-one can get a job based on temporary registration.
 
Kenya nawaaminia mkiamua mmeamua,, sisi huku wenzenu kina bashite ni zero tupu.
 
Watangaze hizo kazi online watu waombe kazi, watengeneze CV. Hata baadae ukirudi Tanzania unakuwa ume make mone na kuongeza ujuzi.

Kwanza si wataajiriwa pamoja na wakenya wapya, unabadili tu kiswahili unaongea kiswahili cha Kenya basi, ama ukiwa kazini huongei kiswahili.

Serikali ya Kenya, itangaze ajira iache mkwara wa kuomba serikali. Mimi mfano nikitaka kuajiri walimu kutoka Kenya natangaza kazi tu naweka wakenya ni eligible kuomba kazi, that's all.
 
Hao MAT wanaleta siasa tu, wao waombe kuhakikishiwa usalama tu, mengine hayawahusu. GoK itangaze tu hizo kazi, kuna vijana zaidi ya 1500 wana njaa huku mtaani, wanafanya kazi za part time na kuchomoa mimba tu, plus huo mshahara ni so tempting, ni mara mbili ya resident wa Tz.
 

Seems the moment unasema kwenda shule miaka Saba sio hoja sijui kwako reward for qualification and meritocracy means anything to you! Doctor's and other civil servants are the real patriots deserving equal compensation accordingly and at our economic capabilities. Not your jubilee and ODM thieves led by jameni nifanye nini ngai! Mimi naweka sahihi tu fellow! Burekabisa! I miss kibaki!
 
Ha ha ha ha haaaaa...nyie jamaa mna vituko!!nnachowapendea Wakenya ni kwamba kuisha kwa huu mgomo ni Madaktari kutimiziwa madai yao basi,naukumbuka mkasa wa tume huru ya uchaguzi.
 

Swala sio usalama wewe!!Hizi taaluma zina ethics zake usifikiri ni kama walimu,hao madaktari wa kenya sio kwamba wanadai kuongezewa maslahi tu bali wanataka pia kuboreshewa mazingira ya kufanyia kazi!!sasa ni daktari gani mwenye akili timamu ambaye angependa kufanya kazi kwenye mazingira magumu?watu wanaheshimu taaluma zao,mazingira wanayofanyia kazi huku kwetu pia ni mabaya na mishahara yao sio mizuri pia kwa madaktari wetu sasa watawezaje kudai vitu hivyo kama wanakimbilia nje?

Alafu ujue hivi vyama vya madaktari vipo kwaajili ya kutetea maslahi ya madaktari na sio kutetea maslahi ya nchi husika,hivyo wao kwenda Kenya ni kama kukisaliti chama cha madaktari cha Kenya.
 
Xplorer kuna madaktari wana njaa vibaya sana mtaani saivi huku, hata ukiwapa kazi kwa 600k - 900k wanafanya kwa roho safi kabisa, MAT hawana msaada wowote kwa hawa vijana wao, saivi mtaani kuna zaidi madaktari 1500 na Oct kuna batch nyingine ya Drs kama 900, hata serikali ikitangaza ajira haiwezi kuchukua hata nusu ya hawa watu tu.

MAT mgomo wa Kenya hauwahusu, kazi yao ni kuangalia well being ya madaktari wa Tz, kama licensed Dr yupo mtaani hadi yupo tayari kufanya kazi kwa 600k Tsh, then unamkatisha tamaa kwenda kuchukua zaidi ya 6m Tsh ni ujinga.

Ushauri wangu kwa GoK, watangaze hizo kazi na rewards zake, Tanzanian Drs watatuma maombi na wataenda kama wakihakikishiwa usalama, mambo ya solidarity wakati familia zenu zinalala njaa si ujanja, na hapa ndio wakenya wanatuzidi ujanja.
 
Plus mazingira ya kazi ya Kenya na bongo hayana tofauti, yote si mabovu tu. Sasa kwa nini Tanzanian Dr akatae kwenda Kenya kwa sababu ya mazingira mabovu wakati ajira anayoililia bongo mazingira ni mabovu hayo hayo, basi agome na kufanya kazi bongo pia.

Tanzanian Drs should focus katika well being yao, mgomo wa Kenya wao hauwahusu, wakachukue pesa hizo hata kama ni kwa short term contract, tumechoka kuona wanafanya kazi za kutoa mimba tu huku mtaani.
 
GoK badilisheni gia angani, badala ya kufanya mazungumzo na serikali ya mfalme haambiliki wa kwetu nyie wekeni Tangazo online tu kisha kwenye terms muandika Tanzanians,Ethiopians and Cuban doctors are only eligible to apply.

Nawaambia kesho tu Kenya itafurika madaktari tena hadi wengine ambao wapo kazini huku kwetu watakuja huko. Muhimu tu ni GoK ijicommit kwenye ulinzi wao .
 
Hao viongozi wengi wa MAT ni waajiriwa tayari kwa hiyo hawawezi kujua shida wanazopata vijana ambao hawajapata kazi
Aliyeshiba hawez kujua shida za mwenye njaa


Nafasi zimetokea vijana watoke wakapige kazi waache kusikiliza porojo za hao jamaa wa MAT
 
Wanasiasa wajanja sana ktk kujitoa kwenye lawama. Kigezo Hapo kwa sasa ni kupanda kwa mshahara na ndiyo maana wanasisistiza tayari wamepandisha ila madaktari hawataki. Ndg zangu Kilichojitokeza mgomo wa TZ uliomjeruhi ulimboka ndio Sawa na huu wa Kenya. Tufuatilie kwa makini maana madai siyo mshahara tu bali pia kuboreshwa kwa mazingira ya Kazi suala ambalo serikali hailiongelei na ndiyo maana wameshindwa kusaini makubaliano. Kama aliweza kununua laptop kwa Kila mwanafunzi wa chekechea hadi shule za msingi kwa nini ashindwe kuboresha mazingira ya health facilities zake? Hata hapa bongo Hospital zote hoi hazina vitendea Kazi unakutana vinavyopimwa ni MRDT na mkojo tu lakini Wanasiasa wanasimama na kudai dawa zipo. Kwa matibabu dawa tu? Sisi raia ndio wa kwanza kushabikia maneno ya Wanasiasa lkn pia ndio wa kwanza Kuumia na kufa tunapougua. Kazi ni kwetu kupambanua yanayojitokeza ila tupunguze ushabiki. Kama Kila boss ktk taasisi za serikali anatumia shangingi serikali inashindwa nini kununua CT scan moja Kila hospitali ya mkoa? Inadhindwaje kupeleka haematological and biochemistry machines ktk hospitali za wilaya???? Issue ni mazingira ya Kazi na siyo salary!!!!
 
Viongozi wa MAT wote wana michongo inayoeleweka, tena wengine hata hawa practise wapo katika NGOs, wameshindwa kuwafikiria kabisa wadogo zao, kama meza ikizungushwa, na Tz ndio kuna maslahi mazuri zaidi wakenya wangekuja tena kwa mbwembwe kabisa. It's only kwa sababu Tz mshahara mdogo ndio maana hatuoni Kenyan Drs huku.
 
Ndio baadae Watanzania watakuja kusema ajira za shida wakati Neema hiyo imemwagwa. Huu ulikuwa wakati wa madaktari wetu kushukuru Mungu na saa wangekuwa wako Kenya
Nimekaa saana Kenya..zaidi ya miaka 30
Nawashauri Doctors wetu wasikubali.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…