Ni jambo la busara kwa madaktari wa Tanzania kuungana kiundugu na hawa wa Kenya, lakini huu mgomo umepitiliza, wengi tuliunga mkono na tukakubali kuumia ili madaktari washughulikiwe kimaslahi, lakini wasemavyo watalaam 'too much of something is dangerous', huu mgomo umekua kero sasa...twafa.
Nafikiri kama sijaelewa vizuri na nipo tayari kusahihishwa, ni kwamba madaktari wanataka kima cha chini cha daktari kiwe Ksh300,000 (Tshs 6,600,000) Lakini serikali imesema kwa sasa uwezo wake ni kwamba daktari wa chini alipwe Ksh.196,989 (Tshs 4,333,758)
Sasa hapo fahari wawili, tutaumia sisi hadi tukome maana viongozi hawana matatizo wao wana hela, wanakimbia kwenda Afrika Kusini na Ulaya kila wakipata mafua.