kuwa serengeti sio kigezo cha kujua kila kitu mkuu
swala la huyu jamaa kuwa na jeshi lake ni tafsiri ya mtaani. Infact nimeshiriki kwenye tafiti kama 4 eneo hilo, na nachoweza kusema ni kwamba bado jamii iko usingizini, mnachofikiria ni poaching tu. Jamaa kawaajiri vijana kutoka jamii zinazozunguka hiadhi yake kama rengers kulinda wanyama wake. Hukusikia ndo yeye aliyeleta faru kutoka africa kusini baada ya miezi kmichache mkamuuwa na kwuchomoka na pembe?
Hawa jamaa wanataka saana kuwaajiri ila hamuajiriki. Kumbuka hii ni biashara na client wake ni watu maarufu. Jiulize kuna vijana hapa kijijini kwenu wakiajiriwa kama hata waiters wanaweza kujieleza kwa ufasaha kwa lugha ya malkia? Je mna lima hata mboga mboga ambazo jamaa angeweza nunua hapo kijijini kwenu?nyama akihitaji let say kg 100 mnaweza supply wa siku? ( amkeni na msisubiri kuamshwa)
kwa kiasi kikubwa watanganyika tumekuwa walalamishi mno, tunabakiwa na kujifariji tu fulani ni fisadi wakati hata tukipewa fursa hatuna tunachoweza ku offer kwa hawa wakoloni. Hawa jamaa wangefurahi tena saana kuajiri receptionist, shef, housekeepers, kutoka vijiji vinavyozunguka lodge yake na mbuga yake mna hao watu?
Nyie endeleeni kupiga siasa badala ya ku confront reality, jiandaeni, kumbukeni hatakuja mkoloni kuwasomeshea watoto na wajukuu wenu, soon jamaa atajenga uwanja wa kimataifa wa ndege mshajiandaa kwa hilo? Au mmejiandaa kwa kulalama tu?