Tanzanian MPs Msigwa na Lema KTN Kenya kuhusu Lissu n.k

Ni kweli na Lissu amesaidia sana kupatikana uwanja wa kusemea maana ukiwa TZ husikilizwi na walioko nje. Naamini wigo wa kupiga kelele (making noise) utapanuka Lissu atakapopelekwa Ulaya au Marekani!
Kila la kheri!
 
Labda nikusahihishe, sijasema ccm kutuma wauwaji Kenya kumshugulikia Lissu, nimesema kama kuna watu wanamtala Lissu kwani Kenya ndio pakijifichia? Napata shida pale watu wanapokuwa wepesi kumeza maneno bila kuweka mbili na mbili. Hivi leo hii ukifanyika uchinguzi na watu huru waka kimilisha kwamba anayrhusika na yaliyo mpata Lissu ni mtu au watu walio ndani ya Chadema, mtalikubali hilo?

Sidhani kama Nyerere au Mandela walikuwa wana watukana viongozi au idara zilozo ongozwa na wakoloni au makaburu kama vile Chadema inavyo tukana na kuwapachika majina ya kifedhuli viongozi wa serikali awamu ya 4 na 5. Kutu ambacho ni chaajabu mama kwa namna moja au nyingine Chadema ni sehemu ya hiyo serikali kwasababu Ina majimbo ambayo inayaongoza na kutegemea fedha za matumizi kutoka hiyo hiyo serikali.
 

..CDM wameomba wachunguzi toka nje waje kusaidia. Lakini serikali imeziba masikio. Wakati huohuo uchunguzi haonekani kuwa na muelekeo wa kuridhisha.

..Wakija wachunguzi huru na wakatupatia majibu mimi nina hakika CDM watayakubali. Ila sina uhakika kama CCM wataweka wazi ripoti za matokeo ya uchunguzi.

..Hivi umeshasahau kwamba Mandela aliunga mkono mapambano ya silaha dhidi ya Makaburu? Au msimamo wa namna hiyo unaona ni mwepesi kuliko huu walionao CDM wa kukosoa serikali iliyoko madarakani?

..Dhana kwamba chama kingine badala ya CCM kikingia madarakani basi wanajeshi, polisi, mahakimu, walioko kazini sasa hivi watatimuliwa kazi hazina ukweli wowote.

NB.

..kuhusu fedha za matumizi kwenye majimbo yanayoongozwa na CDM sijui kama ulifuatilia hoja za waziri Mh.Jenista Mhagama akiungwa mkono na Spika Ndugai kwamba serikali inapaswa kutokupeleka bajeti ya maendeleo ktk majimbo yanayoongozwa na CDM kwasababu wabunge wao waliipigia bajeti kura ya hapana.

..Je hiyo ni HAKI?
 

Hata hao wachunguzi wa nje wakija watataka kuongea na mtu aliye kukuwa na Lissu mara ya mwisho kabla ya tukio ambaye ni dereva. Sasa sijijuwi hata kama ni polisi wa Tanzania wataanzia wapi kufanya huo uchunguzi ikiwa CDM inafanya juhudi za kila aina kumfisha huyo bwana. Kitu ambacho CDM haijakiweka bayana ni nani atalipia gharama za wachinguzi kutoka nje? Maana sioni serikali tena ya kubana matumizi ya JPM kutoa pesa kulipia kitu ambacho serikali inauwezo wa kufanya na ina haki ya kikatiba kufanya. (ndio yale ya kwenda Nairobi wakati muhimbili wana uwezo wakufaya kilichofanyika Nairobi).

Japo unasema waziri Mhagama ameshauri majimbo ya wapinzani yanyimwe pesa, hakuna sharia yoyote inayokubalina na mambo kama hayo. Mara nyingine kila mkoa unataarisha mipango yake ya maendelo na kuwasilisha hazina, hazina inapanga bajeti na kuona kama mipango hiyo itatoa tija kwa wananchi au ni muhimu kufanyika kwa wakati huo. Vyote hivi vinajadiliwa wakati wa mikutano ya bunge na kamati zake. Lakini tukiwa na wapinzani wanaotoka bungeni kila mara wanapo kasirishwa, unategemea nani atawatetea hoja zao?
 

..serikali hii haibani matumizi.

..wangekuwa wanabana matumizi wasingeanzisha miradi isiyo na tija kama ujenzi wa uwanja wa ndege Chato.
 
..serikali hii haibani matumizi.

..wangekuwa wanabana matumizi wasingeanzisha miradi isiyo na tija kama ujenzi wa uwanja wa ndege Chato.
Haha, kuna siku mtakuja kukubali kama walifanya jambo maana kujenga huo uwanja, ni tofauti na mnavyo fikiria. Nuff said
 

..kwanza dereva naye ni mhanga wa shambulizi lile.

..kwa hiyo nakubaliana na wewe kwamba ni shahidi muhimu katika jaribio dhidi ya maisha ya TL.

..kinachonitia wasiwasi ni attitude ya RPC wa Dodoma wakati akitoa taarifa za kumtafuta dereva wa TL.

..zaidi ya dereva, TL naye ni shahidi muhimu ktk tukio zima.

..Swali la msingi ni kama Polisi ambao kwa muda mrefu wamekuwa wakimkandamiza na kumsumbua TL, je ghafla wanaweza kubadilika na kumtendea haki?

..Nakubaliana na wewe kwamba madai ya Waziri Jenista Mhagama kwamba majimbo yenye wabunge wa upinzani yasigawiwe fedha za bajeti ya maendeleo hayana msingi wowote wa kisheria.

..Lakini cha kusikitisha ni kwamba alitoa tamko lile bungeni. Pale alikuwa akizungumza kwa niaba ya serikali. Wakubwa zake hawakumsahihisha ndani wala nje ya bunge.

..Kwa hiyo utaona kwamba kuna imani inajengwa kwamba wapinzani hawastahili haki sawa na ndugu zao wa CCM. Wapinzani wamegeuzwa maadui wa nchi hii.
 
Wengi wetu tunajuwa utaratibu unaotumika kama kuna tukio lolote lile, liwe ni ajali au uhalifu. Lazima polisi waarifiwe na kuandikisha maelezo (statement) ambayo ndio itatumika kama kielezo cha kwanza uchunguzi unapoanza.

Tunaambiwa dereva wa Lissu anapata matibabu ya kisaikolojia Kenya, bila hata uthibitisho kama ni kweli alihitaji matibabu hayo maana hajachunguzwa na mtaalamu yoyote wa hapa nyumbni kama vile Lissu alivyopata huduma ya mwanzo Dodoma. Nashamgaa hata polisi kwanini wasimuhoji huyo dereva pale pale Dodoma na wakaacha mwaya wa yeye kupenya na kuenda Nairobi.

Japo unasema kwamba Lissu amesumbuliwa sana na polisi inawezekanaje leo polisi wakamtendea haki. Hata mwizi anaeshinda akifukuzana na polisi kila siku, akipata janga abalo linahitaji msaada wa polisi atajipeleka mwenyewe polisi. Mimi naimani pamoja na hii picha Lissu alikuwa anajaribu kichora kabla ya tukio kwamba polisi ni adui wake, moyoni anaimani kubwa na polisi. Maana polisi ni watu anafanya nao kazi kila siku katika kesi zake anazowatetea watu wengine.

Nikija kwenye swala la mama waziri, na kama wapinzani ni maadui wa nchi hii, kwaupande wangu mimi najuwa kama huu ni mchezo wa kisiasa. Inawezekana kabisa waziri alisema hayo akijuwa kama kauli kama hiyo haita pita bungeni lakini kasema tuu kuwachokoza wapinzani. Wanasiasa wa sura mbili wakiongea na kadamnasi, sura moja ni ya kujionyesha kwa wafuasi wake kama yeye ndio kinara, na sura nyingine ni ya kikazi ambayo sio ya mchezo mchezo. Mfano rais Kenyatta aliposema atawashugulilia majaji walioamua kesi yake. Kama unaelewa siasa pale alikuwa anawajaza imani wafuasi wake kama yeye ndio mwanaume na hakuna wa kumtisha, lakini kiuhalisia hana nguvu yoyote ya kuwashugulikia majaji kisheria. Na ndio maana unaona hata Lissu alijuwa kuwa kama anafuatwa na magari asiyo yajua alitakiwa atoe taarifa polisi ili uchunguzi ufanyewe, lakini yeye aliemda moja kwa moja kwa waandishi ili kupata maximum impact huku anajuwa kama polisi ni lazima uwafate wewe au uwaite kwenye eneo la tukio.
 


..nadhani CDM wanaamini POLISI au vyombo vya dola vimehusika na tukio hili. Na ndiyo maana hawawapi ushirikiano unaotarajiwa ktk matukio kama hili lililotokea.

..Mimi nadhani tusubiri tu MUNGU akimjalia TL afya basi atakuja kueleza ukweli wote.
 
Ni kweli kwamba Lissu, CHADEMA na dreva hawana imani na polisi. Na ndiyo maana kwa makusudi hawakutoa taarifa polisi ya ama kufuatwa na hiyo wanayodai kuwa ni Nissan nyeupe au juu ya nyendo za hao wanaodaiwa kutekeleza unyama huo kwa Lissu, ingawa walikuwa na muda wa kutosha (zaidi ya dakika 20). Na hata kama hawakuwa na haja ya kuitaarifu polisi, basi walikuwa na muda wa kutosha kuwajulisha viongozi wao au kuitisha kikao cha waandishi wa habari!
Kuhusu bajeti, kama wabunge wa upinzani wamekataa kupitisha bajeti, je fedha ya kupeleka majimboni kwao itatoka wapi? Na je, watakuwa na haki ya kufuatilia mwenendo wa bajeti hiyo iliyopitishwa na upande mmoja wa wabunge?
Ni kweli pia kwamba, upinzani wa kweli huhoji kwa hoja na si kwa matusi. Ukishatukana ni dhahiri kwamba umepanda chuki katika uhusiano wako na huyo unaemtukana na matokeo yake ni mahusiano mabaya (na ambao nauona kama mtaji wa kisiasa). Kwa maana nyingine 'mkono mmoja huosha mwingine' Ubaya kwa ubaya, uzuri kwa uzuri! Uhusiano si wajibu wa mtu au upande mmoja! Ni wajibu wa wote!
Tujitafakari!
 
Duh, hivi watz mlifika huku vipi, upinzani umekua uadui sasa mmeanza kuwindana kabisa...2015 nlikuwa tz na hali ya hewa chini ya mjomba ilikuwa nzuri tu, mnabishana alafu yanaisha freshii ila sasa hivi yaaani....poleni
Siku baba yako akiugua ugonjwa wa akili huku kashika panga utajua tumefikaje huku
 
Siku Kenyatta akipata matatizo ya akili akiwa ikulu utajua tz inapitia wapi
 

TUJITAMBUE, WAKATI NDIO HUU
wapinzani wamefanya nini

1. wamepinga na kuzuia miswada mibovu inayonyonya nchi yet na kutuacha maskini hivyo mmi na familia yangu tumeepushwa na janga hilo pia

2. wameibua ufisadi mkubwa dhidi ya uchumi wetu mfano epa dowans meremeta tegeta escrow lugumi nk hivyo kwa kuibua ufisadi serikali ambao ulisaidia serikali kukomboa mabilion ili yakajenge brabara na zahanati ambazo mmi n familia yangu tunatumia

3. Upinzani umeisimamia sana serikali kwa kukosoa na kushauri mfano safari za nje pia ukubwa wa araza na mengineyo ambayo yameifanya serikali ijirekebishe kwa kuwajibika na kuacha udhaifu huo hivyo kuokoa pesa zilizojenga miradi kibao ambayo mmi na familia. yangu tunatumia

pia wametoa mawazo mbadala ambayo mengine serikali imeyachukua ili kuongeza ufanisi mfano miaka mingi chadema ilidai posho nyingi ni mzigo kwa serikali hivyo ni muhim kubana matumizi tumeona wazo lile la dr slaa linatumika ssa hivyo kwa namna moja ama nyingine linanufaisha familia yangu sababu pesa ilioikolewa itajenga miradi kibao

je niongeze ama inatosha??
 
Ni kweli na Lissu amesaidia sana kupatikana uwanja wa kusemea maana ukiwa TZ husikilizwi na walioko nje. Naamini wigo wa kupiga kelele (making noise) utapanuka Lissu atakapopelekwa Ulaya au Marekani!
Kila la kheri!
inaonekana huna ujuzi na mambo ya kidiplomasia na kimataifa kuona mtu kukosoa serikali yake kwenye platform ya kimataifa ni big deal!!!si nmekupa mifano ya waliowahi fanya alichofanya msigwa umeufyata!!

anyway ukweli ni kwamba unapoonewa na kukosa msaada ni lazma tu utafute msaada nje hta nyerere alienda na marealle UN na kukosoa serkali ya ukoloni pia Mandela alikuja Tanzania kuikandia serikali yake ssa kma hao walifanya who is Lema???
 
zitto junior, ni vyema kuorodhesha mabaya yaliyofanywa na Serikali za CCM kwa miaka yote tangu uhuru, lakini bila kutoa pongezi kwa Serikali ya CCM iliyoko madarakani sasa kuanza kuyatekeleza kwa vitendo.

Kwa sababu hiyo sioni tatizo mimi kuwaitaa viongozi wa upinzani ni kuwa ni wanafiki. Unafiki wao ni kukebehi juhudi za Serikali iliyoko madarakani, kutekeleza kwa vitendo hayo wanayodai waliyaibua wao. Unafiki wao unazidi pale wanaposhindwa kutofautisha nani mkweli kwa Watanzania, kati ya wao mabingwa wa kukosoa na kurukia matukio, na Serikali inayojibu kero za wananchi kwa vitendo (maji, barabara, huduma za afya ya jamii, elimu, uchumi, nk).

zitto junior, nikushukuru kwa kuwa muwazi na mkweli kuorodhesha kero za wananchi zinazotekelezwa na Serikali - leo Waziri Mkuu anaweka jiwe la msingi la mradi mkubwa wa maji, Longido. Jana Rais amefungua barabara ya kwenda kwenye machimbo ya madini ya Tanzanite na kuagiza eneo hilo lilindwe kwa kuwekewa uzio. Kama siyo kuthubutu kwa Serikali utasema nini?
 

Kufyata maana yake ni kunyamanza? Hizi sio hoja za mtu na mtu. Ni hoja za wanafamilia wote wa JF. Na hatushindani kwa kupiga kelele bali kwa kupaaza sauti!

Kuna ukosefu wa maarifa lakini pia kuna uwezo wa kupambanua mambo usiokuwa na maarifa nayo. Au unafikiri siwezi kutofautisha kati ya pikipiki na baiskeli nikiviona? Kimsingi sijakataa ukosoaji kwa kutumia majukwaa ya kimataifa kwa sababu kufanya hivyo kunakuwa na jukwaa huru la kubaini ukweli kimataifa. Ndio maana nikasema, hii ni fursa nzuri kwao na kwamba Lissu atakapopelekwa Marekani au Ulaya, watakuwa na fursa nyingine ya kupiga kelele (making noises and not raising their voices) kwa kutumia vyombo vya habari vya huko km CNN, Aljaazira, BBC, nk.

Ukinipa mifano ya Nyerere kwenda na Mareale (?) UN na Mandela kuja Tanzania maana yake ni kutaka kuniaminisha mimi na wengine kwamba nchi iko kwenye mapambano ya kudai uhuru. Na kama ndivyo, mimi simo na nakuomba usipoteze muda wako kwa hilo! Naamini tuko kwenye mabambano ya kiuchumi ambayo ni vita yetu sote.Jiunge!
 
mkuu kwanza ningependa nieleze kusikitishwa kwangu na supporters wa serikali yaani wao kila ukionyesha udhaifu wao wanakimbilia kueleza mafanikio yao mfano magufuli akiitwa dikteta utaskia ooh kajenga reli sijui kazuia wizi wa madini ssa najiuliza toka lini uadilifu unafunikwa kwa uchapa kazi?? hivyo nsingependa kuona na wwe unangukia kwenye mtego huo yaani tujibu hoja iliopo mezani maana no matter how akiwa mchapakazi inapunguza ukweli Kuwa ni dikteta kwa kuwabana upinzani??

2. WAPINZANI WANADANDIA MATUKIO huku serikali inatekeleza kwa vitendo. Hivi kudandia matukio ndio kupi?? nachojua upinzani upo kuicheck serikali yaani kila inachofanya serikali lazma upinzani utoe msimamo ndio maana hata bungeni serikali ikileta bajeti ni lazma upinzani ujibu kwa bajeti kivuli sasa kudandia matukio hakupo zaidi hiyo ndio moja ya kazi za upinzani

3.WAPINZANI WALIOSEMA NDIO YANATELEZWA hivyo unaona ni wanafki ssa nikuulize je unaposema elimu ina ubovu then mnasema tuiinue alafu awamu ya tano inakuja na agenda ya madawati hivi kweli wasifie??? mfano mwingine wakasema miswada ya madini ni mibovu kweli magu akasema ifanyiwe marekebisho alafu ghafla eti yanaletwa kwa hati ya dharura je ulitegemea upinzani wasifie ??? SHIDA SIO ULICHOKITAKA SHIDA KIMETEKELEZWA KMA ULIVYOTAKA???

kweli kuna mambo mazuri serkali imefanya na tunatoa pongezi ila ni kodi zetu ssa unaposema eti upinxani wanaongea hku serikali inatekeleza ulitegemea upinzani wajenge SGR?? kodi tunawapa serikali ndio maana wao wanatakiwa wasimamie maendeleo hao upinzani kazi yao ni kusimamia uwajibikaji wa serikali na kuikumbusha inaposahau ssa kivp unategemea upinzani uanze kununua bombardier na kujenga Barbara wakati hawapokei lolote zaidi ya ruzuku tu! is that fair
 
Ni ukweli usiopingika, kikatiba, kwamba mmoja ya kazi za Bunge (sio upinzani) ni kuisimamia serikali na kazi ya upinzani ni kuikosoa serikali, jambo ambalo ni nzuri kwani sisi kama nchi, tumeridhia kuwa na mfumo huo wa vyama vingi.
Aidha serikali nayo inapaswa, kwa namna mmoja au nyingine kutafakari kwa kina ushauri au ukosolewaji unaofanywa na, si na upinzani tu, bali na bunge na wadau wengine wote wa maendeleo ndani na nje ya nchi. Ni katika mktadha huo tunapoweza kupiga hatua za maendeleo kwa kasi inayohitajika kwani nchi hii ni yetu sote.
Nisichokubali ni kule upinzani kutaka serikali inakili neno kwa neno (copy and paste) ya kile wanachoshauri / kupigia kelele na pale kinapotekelezwa kinakuwa ndio mtaji wao wa kisiasa majukwaani bila hata kuonesha dalili ya kufurahia kilichofanyika (no sign / word of appreciation) na serikali!
Vinginevyo, big up sana upinzani (sio wapinzani wa matusi na majigambo)!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…