Marhaba...
Mkuu nimekupata , ila bongo nimetembea Dar kwa wiki moja tu nikiwa pamoja na rafiki yangu mmarekani,kama mtalii vile ila sikujichanganya maana nilijifungia hotelini usiku kucha ,mchana kutwa wiki nzima,kwa kuwaogopa wabongo.😛
Arusha pia nishafika na kugeuza baada ya siku moja tu....sikupapenda pale,yaani huduma ilikua duni kiaina.
Tukashauriwa twende sehemu za Tanga tukapate burudani lakini kwa hali zilivyo barabara kwetu Afrika ,ilitulazimu kugeuza hadi Nairobi tukakwee pipa.
Wakati huo KQ alikuwa mbabe wake PRECISION AIR na pia pesa zilikuwepo $$$ za kumwaga(Mastercard) ,mwendo wa kula bata kwenda mbele.
😀😀!
Hata hivyo ni dhahiri mtu akilelewa jijini ,huwa hadhuriki na kilugha ya asili kirahisi ,pia ni mtihani kuujua asili yake.
Siku hizi binadam tumechanganya damu bwana wee!...acha tu!
Mimi hap nna jamaa wenye asili ya kihabeshi/kisomali upande wa baba na luo wa Kenya/Tz/busoga kule uganda upande wa mama....mchanganyiko wa ajabu.
Babu alikuwa mfanyabiashara mashuhuri na alikatiza hadi sehemu za Uganda kule ,Kilifi pamoja na Lamu.
Naomba nikomee hapo nisije nikaubughdi kadamnasi.