Tim Choice
JF-Expert Member
- Sep 28, 2013
- 2,088
- 1,261
😀😀😀😀Wapi bana, vitu anayovichora Kipanya havijakaribia Gado, akithubutu kumuiga Gado mnamnyongea baharini. Hapo kwenu mnakamata upinzani kisa wametoa msaada kwa wahanga wa tetemeko la ardhi. Najaribu kupata picha eti akina Raila Kenya wanakamatwa kwa kupeleka msaada kule Turkana ambapo kuna kiangazi.
Hivi kumbe Tim Choice huwa ni mkenya! Mbona unaandika kiswahili vizuri kuliko wakenya wengine?
Oh, mnapo kuwa TZ mnajiona kama mko Nairobi. See wewe ndio mkenya peke mwenye akili hahaNairobi iko TZ
MK254 sijui nawe wasemaje?...nipo fiti mkuu ama bado?
Uko fiti bro, japo kuwa mkweli lazima kuna kipindi umeishi Bongo. Binafsi nakiri ujio wangu Bongo uliniwezesha kuboresha jinsi ninavyo ongea Kiswahili. Halafu ukizingatia mimi mzawa wa mjini, hivyo lafudhi yangu huwa sio rahisi kujua kabila/asili yangu kabla sijakutajia jina langu.
Kuna siku tulipiga siasa za Kikenya na Wakenya sehemu Nairobi, halafu baada ya muda mrefu jamaa wakaanza kuniuliza na vipi huko kwenu tunaskia Magufuli ni noma. Yaani jamaa hawakunishtukia kwamba mimi Mkenya kwa muda wote huo japo nilidhihirisha uelewa wa ndani wa siasa zetu. Wao walidhani mimi ni Mtanzania ambaye anafuatilia mambo ya Kenya.
Pia uhamiaji Kenya washanizingua sana kipindi nafuata kuongeza muda cheti changu cha usafiri/passport renewal. Ilinilazimu niongee kilugha changu cha asili tena kwa ufasaha ndio jamaa wakafuta mashaka yao kwangu.
Sasa vioja huwa pale nikiwa Bongo halafu jamaa wasionifahamu waanze kuongea kuhusu Wakenya. Yaani wataongea kwa muda wote bila kunishtukia. Kuna demu niliwahi kumpeleka out pale Mwanza, hakuwa anajua mimi Mkenya, muda wote aliwasimanga Wakenya waliokua wanapata burudani pembeni. Nilimtema baadaye maana alionyesha kuwa na chembe za ubaguzi, lakini hadi tunatoka pale, hakuweza kunishtukia.
Huwa napata raha kuishi hivyo, bila mtu yeyote kung'amua asili yangu, iwe kwa Wakenya au Watanzania. Japo nikitembelea kijijini naongea kilugha changu cha asili tena kwa raha. Hata mjini nikiwa na ndugu zangu.
Mk254 na Tim choice swala la kisw nmewakubali mko vyema kabsa... ..vipi nikija Kenya ni kitu gani kitachofanya nigundulike kirahisi kua mimi ni mtz? ?? Kama ni lugha naongea kiswahili na kingereza
Marhaba...
Mkuu nimekupata , ila bongo nimetembea Dar kwa wiki moja tu nikiwa pamoja na rafiki yangu mmarekani,kama mtalii vile ila sikujichanganya maana nilijifungia hotelini usiku kucha ,mchana kutwa wiki nzima,kwa kuwaogopa wabongo.😛
Arusha pia nishafika na kugeuza baada ya siku moja tu....sikupapenda pale,yaani huduma ilikua duni kiaina.
Tukashauriwa twende sehemu za Tanga tukapate burudani lakini kwa hali zilivyo barabara kwetu Afrika ,ilitulazimu kugeuza hadi Nairobi tukakwee pipa.
Wakati huo KQ alikuwa mbabe wake PRECISION AIR na pia pesa zilikuwepo $$$ za kumwaga(Mastercard) ,mwendo wa kula bata kwenda mbele.
😀😀!
Hata hivyo ni dhahiri mtu akilelewa jijini ,huwa hadhuriki na kilugha ya asili kirahisi ,pia ni mtihani kuujua asili yake.
Siku hizi binadam tumechanganya damu bwana wee!...acha tu!
Mimi hap nna jamaa wenye asili ya kihabeshi/kisomali upande wa baba na luo wa Kenya/Tz/busoga kule uganda upande wa mama....mchanganyiko wa ajabu.
Babu alikuwa mfanyabiashara mashuhuri na alikatiza hadi sehemu za Uganda kule ,Kilifi pamoja na Lamu.
Naomba nikomee hapo nisije nikaubughdi kadamnasi.
Media za kenya hupenda kushobokea watu sanajibu ni moja tu,JPM hategemei umaarufu wa kupitia social media,ni uchapakazi wake ndio unasababisha ajadiliwe ktk social media kila sehemu duniani.
Uhuru Kenyatta anategemea umaarufu kupitia social media kwa 100%.ndio maana kila anachofanya lazima aweke update Fb na twitter ili watu wamsifie.
Kushangaa nyumba sio rahisi. .....mashalaah dar nimjini kiasi kwamba nmeoshaa macho vya kutosha ....kutembea taratibu inategemea niko na nani besides. ..naenda wapi pia. ..kiswahili unaongea pale unapohisi uyo utaezungumza nae mtaelewana so nahisi hamna peculiar character to distinguish a Tanzanian from you buddies ....Jikokote mwendo wa kobe utembeapo mjini huku ukishangaashangaa majengo pamoja na kiswahili ndefu(yaan maneno mengi..bla,..bla..bla)hapo utatambulika tu kama mtz!..teteheheh!....nakutania tu mkuu!....😀😀
Mkuu ntakujibu kesho, muda umekwisha naondoka sasa ofisini.
MK254 si wajua leo ni mwisho wa mwezi lazima wakenya walioko nje ya nchi na bara "(diaspora)" wakafanye ibada tukufu( kutuma hela)...tukaijenge Kenya yetu tukufu!
Itabidi niiwahi Western Union mapema.
Sijui kwa nini hamna MPESA huku, nakereka kweli kweli.
Media za kenya hupenda kushobokea watu sana
Ona hii
Mbwembwe zinazomsubiri Magufuli Ikulu ya Nairobi
Poa Mkuu ila sie huku Bongo imetokea ajali mbaya sana ya Bus la abiria na Gari kubwa la Mizigo,Jioni njema maswahiba!.........usiku mwema.....huku tayari ni saa mbili usiku!
MOTOCHINI,
Inabidi hawa swahilihub waombe msaada wa MK254 au Jamiiforums ili kupata mwendelezo wa habari ya ziara rasmi ya kiserikali ya Magufuli maana Kiswahili kinawapiga chenga wanategemea 'Google- Translate' , nimenukuu hapo chini:
Rais wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli.
Na VALENTINE OBARA
Imepakiwa - Sunday, October 30 2016 at 15:13
Kwa Mukhtasari
KENYA itamwandalia Rais wa Tanzania John Pombe Magufuli dhifa Ikuluni licha ya kuwa kiongozi huyo ana sifa ya kupunguza matumizi ya pesa kwa karamu za kitaifa nchini mwake. Mbwembwe zinazomsubiri Magufuli Ikulu ya Nairobi
MOTOCHINI,
Inabidi hawa swahilihub waombe msaada wa MK254 au Jamiiforums ili kupata mwendelezo wa habari ya ziara rasmi ya kiserikali ya Magufuli maana Kiswahili kinawapiga chenga wanategemea 'Google- Translate' , nimenukuu hapo chini:
Rais wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli.
Na VALENTINE OBARA
Imepakiwa - Sunday, October 30 2016 at 15:13
Kwa Mukhtasari
KENYA itamwandalia Rais wa Tanzania John Pombe Magufuli dhifa Ikuluni licha ya kuwa kiongozi huyo ana sifa ya kupunguza matumizi ya pesa kwa karamu za kitaifa nchini mwake. Mbwembwe zinazomsubiri Magufuli Ikulu ya Nairobi
Aende salama na Arudi salamaTaarifa rasmi kutoka Ikulu ya Tanzania.
View attachment 426767