Jinsi ya kupika biriani tamu ule ujirambe .
Beef biriani.
Mahitaji.
Nyama kg 1
Basmat rice kg 1.
Vitunguu maji robo 3 .
Paste yenye vitunguu swaumu,tangawizi ,kotmiri. Kiasi cha robo kikombe.
Mtindi kikombe 1 cha chai.
Biriani masala vijiko 2 vya chakula.
Garam masala kijiko 1 cha chakula.
Food colour ya kuweka kwenye wali wako wa biriani/orange.kiasi cha kijiko 1 cha chai.
Viazi mbatata kiasi cha robo kg.
Nyanya kg 1
Nyanya paste robo kikombe cha chai.
Matayarisho.
Chukua nyama yako ambayo ushaiosha weka kwa sufuria halafu tia nyanya uliosaga,paste ya kitunguu swaumu,mtindi,nyanya za kawaida na ile ya paste,masala zote za biriani,na chumvi acha zikae kwa nusu saa zikolee viungo.
Kwenye karai kaanga vitunguu vyako mpaka viwe vya brown ila hakikisha usiunguze ukimaliza kukaangaa vyote sasa chukua ile nyama yako uweke kwa moto acha itokote mpaka uhakikishe imeanza kuiva ndio unaweka sasa vitunguu vyako ila acha kidogo vitunguu kwa ajili ya kuweka kwa wali wako.
Pika rojo lako mpka utakapoona limeanza kuwa zito sorry nilisahau viazi ,vile viazi vikate pande 2 kisha vikaange vikishaiva kiasi ndio uchanganye na lile rojo lako likiwa tayari epua tayari kwa kulia na wali wako.
Jinsi ya kupika basmat rice .
Roweka mchele wako kwa lisaa 1
Ukimaliza chukua sufuria yako tia maji ya kutosha yawe nusu ya ile sufuria kisha weka kwa moto na hakikisha yakishachemka ndio uweke mchele wako pamoja na chumvi acha kwa dakika kadhaa ila usiive sana halafu mwaga maji yote ,chukua mafuta yale uliyokaangia vitunguu kama vijiko 3 tia kwa ule wali wako koroga halafu weka rangi ya biriani kijiko 1 cha chai weka kwa kikombe na maji koroga,sasa nyunyizia vile vitunguu ulivyokaanga kwa wali na kama una mdalasini nzima weka kama vijiti 3 kisha wali wako funikia kwa moto mdogo wa chini mpka uhakikishe umeiva.