Idea inaweza kuwa nzuri, lakini kwa jinsi ulivyoandika bado sijaona kama inatekelezeka. Kama utafafanua jinsi unavyoforesee outcomes za huo mkutano inaweza kusaidia kuelewa umuhimu wake. Nionavyo mimi ni kwamba kama kweli lengo ni kuhusisha diaspora basi hakuna better venue than internet, otherwise hatutakuwa na mkutano wa diaspora kwa maana sahihi.Na ninachojiuliza haswa ni swali hili, je ni nini kinakosekana sasa ambacho kitapatikana kwa kufanyika mkutano huo? kwa sababu kumeshakuwa na mikutano ya aina hiyo ukiwepo ule wa London lakini mpaka sasa hakuna utekelezaji wa maamuzi wernye kuleta mabadiliko mazuri kwa diaspora.
Mzalendo ZeMarcopolo,
Nashukuru sana kwa maoni yako mazuri na mapendekezo mbadala. Ungesoma kwa makini post kuu na michango ya wengine hapa, ungeona majibu ya maswali yako. Hata hivyo nitajitahidi kukujibu:
Outcome:
Hii itategemea jinsi wajumbe watakavyoamua na kukubaliana lakini inategemea pia na resolutions. Ya kwangu machache ninayofikiria binafsi ni haya:
- Kama TPN inavyofanya sasa, inawezekana kuanzisha serious business ikiwa na Partners kutoka Diaspora na wale waliopo TZ on a serious note. Role ya Diaspora partner ikiwa ni kuangalia masoko ya nje (kama biashara hiyo ina hilo), kuchangia mtaji, mawazo ya kibiashara nk.
na partner wa nyumbani kuendesha na kusimamia biashara. TPN inaweza ikaguarantee usalama na uaminifu wa wote kama kiungo.
- Moja ya malalamiko toka Diaspora ni kuwa TZ hakuna serious people to Trust. Kuna ambao wametuma pesa wajengewe, haikutokea, kuna ambao wanatuma pesa kwa mambo mbalimbali lakini bado kuna matatizo. Tunapenda kuona TPN inakuwa kiunganishi muhimu cha vitendo na kuleta mafanikio kama ambavyo inatokea sasa.
- Kunaweza kuwa na kuanzishwa kwa Databank and Labour & Business Exchange Centre on a serious note. Kuna Diaspora ambao wangependa kurudi nyumbani lakini hakuna basic information ya uhakika ya nini wanaweza kufanya wakirudi bila kuteteleka. Databank inaweza ku-provide practical details in the real current situations, business opportunities, partners, nafasi za kazi nk.
- Kuongeza kasi za kufungua Chapters au kuwalink wa TZ na Diaspora kupitia jumuiya zao kwa mambo yote muhimu ya kujiletea maendeleo.
- Wenzetu wa jamii ya Kiasia hapa TZ wana Jumuiya zao km Majamatini n.k. ambako huko wanapeana mitaji na masoko ya biashara wakati sisi inatuwia vigumu kusaidiana kwa hilo. Tunaweza kufanya Summit ikawa kama market place na mahali pa masoko.
- Tunaweza kuanzisha bank/fund yetu on a seriuos note. Niliona resolution hiyo kama hiyo summit ya UK ingawa sijui utekelezaji wake umefikia wapi maana wizara ya mambo ya nje pia hawajui. TPN imeshaanzisha fund tayari. Inahitaji kuboreshwa. Kwa mtazamo wangu inatakiwa team work ya waliopo ndani na nje ya nchi kufanikiwa zaidi katika hili.
- Kuanzishwa kwa mtandao mkubwa ambao unaweza ukawaunganisha wa TZ wa ndani na nje katika mambo ya kibiashara, masoko na mengine ya kuleta maendeleo.
- Kubadilishana uzoefu katika sekta mbalimbali, nk.
Binafsi ndoto yangu ni kuona Watanzania Wasomi na Wanataaluma wanaweza kujijengea uwezo wa kibiashara na kimitaji ili kuboresha maisha yao na kuleta maendeleo.
Juu ya hoja yako ya Internet Forum /Sumit. . . Ndugu yangu ni wazo zuri lakini utashangaa sana nikikwambia kuwa TZ walio na Access na Internet hawafiki hata laki tano. Na katika hao sijui ni wangapi wanaoweza kufika katika ONLINE FORUMS kwa kukosa nafasi, kukosa wakati mwafaka na hata uwezo wa kutumia. Pia si wengi ambao wanahamasika kwa njai hii. Mfano mdogo ni idadi ya wale tu ambao wanatembelea JF na hata thread hii. JF ina wanachama karibu 6000 lakini active kwa siku sidhani kama wanapita 1000 na katika thread hii hata 500 hawaajafika mpaka sasa.
Nia ya kukutana pamoja TZ (Si UK au USA nk) ni pia kupata kujua hali halisi ya Tanzania wakati tunaongelea mambo haya kwani wadau wote muhimu tutawaalika. Pia face to face meeting with potential partners wa ndani na nje ya nchi n.k.
Pia inaweza kuwa ni nafasi ya kuyafanyia kazi mapungufu yote yaliyotokana na summit kama hizo zilizofanyika huko nyuma.
Kama una mawazo zaidi ya kuboresha au hata mbadala yanayoweza kufanya kazi, tuendelee kushauriana ndugu yangu.