mulisaa naona umefunguuuuka mwenyewe, ila vizuri kuongea ya moyoni maana lake mtu halimtapishi..
furaha na hali ya siasa sehemu fulani kwa namna moja ama nyingine inachangia kwenye hilo jambo...
furaha ya mtu na hali ya demokrasia sehemu fulani inaweza kuchangia kwa namna moja ama nyingine...
binafsi, Tanzania kwa sasa hatujafikia hatua ambayo tuseme ndo tupo dhofu li hali kwenye suala la furaha...
mtu ataikubali hii taarifa kwa kuoanisha hali ya demokrasia na siasa kwa ujumla nchini, atatolea mfano wa Tundu Lissu, Akwilina Akwelina(R.I.P), Ben Saanane, Azroy n.k
hiyo ni baadahi ya mifano tuu, sasa kwa mifanp hiyo kwa namna moja ama nyingine utasema ni kweli Tanzania hakuna kitu kinachowafanya wafurahi kwa kua hali si shwari nchini...
kwani zipi ni viashiria vya furaha kwa binadamu, siasa na demokrasia pekee??
binafsi ili nisiwe na furaha, matatizo ya kifamilia, mienendo ya kibiashara au masomo kwenda kombo, kushindwa kufikia malengo kadhaa, masuala ya mapenzi n.k...
sasa mulisaaa umekuja hapa kumwaga mchele kwenye kuku wengi, tena kuku wenyewe ni broila...
fujo walizozileta hapa ni zaidi ya kutaka kujua kwanini hatuna furaha...
umefurahisha baraza hongera kwa hilo pia
Binafsi Mimi nina furaha, hakuna kinitatizacho kwa sasa mpaka nisiwe na furaha, nimemuuliza Mama yangu pia ameniambia ana furaha pia...