Ni kweli usemavyo.
Kwangu imekaa kamavile CCM wameingiliwa na sisi akili zetu zimekufa Ganzi???
Ngoja nichangie kwa kupotoka kidogo.
Nasikia anaye sadikiwa kuwa
MchapakaziNamba moja wa CCM Edward Lowassa aliyetuingiza kwenye Issue ya
Richmond na Dowansa na yeyey kuondoka na Kitita cha kununua kila mtu kwenye system,amefufuka kutoka miongoni mwa WAFU akiwa na Rungu mkononi tayari kuwania
kiti cha Urais mwaka 2015.
Edward Lowassa hatakiwi kuachiwa ktimiza dhamira yake chafu.
Uchapakazi kazi wake si positive kwa sababu unaenda sambamba na Uharamia, hautuutaki hata Bure. Edward Lowassa ametumia muda wake mwingi kujenga Himaya ya MAFIA Tanzania na kuilinda kwa nguvu za kiserikali na PESA ya Wizi
Majambazi nao hukaa chini na kupanga mikakati kwa masaa mengi kabla ya kufanikisha. Ni wachapakazi, lakini wachapakazi ya kurarua, kubomoa na kuharibukila kitu.
Sidhani sis kama watanzania kwa ujumla wetu hatuna akili kiasi cha kudharau tatizo la nishati ya umeme.
Kuna matatizo mawili makubwa niyaonayo pengine ndiyo chanzo cha Watanzania kutokuwa na nguvu ya pamoja ya kupigana kwa nguvu zote kuhakikisha tatizo la umeme linakuwa Historia.Umeme unatumiwa na karibu 6%-9% ya wananchi wa Tanzania na kutokana na mgao umeme at any time t unatumiwa na less than5% ya waTZ. Kwahiyo umeme bado inakuwa si issue ya wengi iwe mjini iwe kijijini.
Watumiaji wa umeme wanatumia kuwasha taa huku wakipika kwa kuni mkaa na mafuta ya taa. Umeme unatumika zaidi kwa mwangaza na majokovu si nishati itumiwayo kufanya kila jambo majumbani.
Kwakidokeza tu,hata suala la maji lina sura inayofanana na hiyo,watu wlaiounganishiwa maji majumbani mwao ni kidogo sana walio wengi wanadandia huduma hiyo hapa na pale. Watu wanao dandia huduma si rahisi kudai huduma hiyo kwa sauti moja
Tukkirudi tena kwenye suala la umeme, kwa vile watumiaji wa umeme ni kidogo kulinganisha na idadi ya watanzania kuna watu wengi mijini na vijijini waonao nishati ya umeme kuwa tatizo lakini si tatizo la kuwagusa moja kwa moja. Watu hawa si rahisi kwao kupiga kele za kudai upatikanaji wa nishati hiyo. Kwa si suala la kufa na kupona.
Kam mwana Mageuzi na nipendayye Positive Change Ninafurahia kwamba Serikali ya CCM inajitengenezea Kifo yenyewe kupitia mabadiliko yanayoendelea kila siku nchini Tanzania.
1 Kasi ya kupanuka kwa miji yetu haiendanii na ukuajiwa huduma zote mijini huduma kama maji nishati ya umeme, mifereji ya maji machafu ,barabara, Usalama wa raia, open space, na usafi.
2 Vijana wasiokuwa na kazi baada yakuhitimu Vyuo vikuu na kidato cha sita wanaongezeka kwa kasi sana, ongezeko lao haliendi sambamba na ongezeko la kazi.
Hayo mawili hapo juu ni Mabomu ya kutosha kuipeleka serikali ya CCM chini.
Yeyote mwenye uwezo wa kutumia mitaji hiyo miwili anaweza kuiangusha serikali ya CCM ndani ya mwezi mmoja bila kutumia nguvu ya chama cha kisiasa dini wala itikadi.
Pengine kabla ya kwenda mbali sana katika suala la NISHATI ya UMEME ni vema tujiulize; Ni nini mataraji ya Mtanzania wa kawaida katika maisha yake??
Je anasubiri zamu yake ifike ili naye aje aibe atajirike kama akina Lowassa na Rostam?
Amekata tamaa na yuko radhi kuishi kwa kuikubali hali yeyote iwayo??
Anajipanga kikamilifu kubadili maisha yake hatua kwa hatua?
Anawaona Viongozi wa serikali ya CCM ndiyo wenye jibu la mwisho la matatizo yake??
Anajua ana matatizo, lakini mengi ya matatizo yanayo mkabiri hata hajui kwamba ni matatizo, na zaidi ni matatizo yaliytengenezwa na uongozi mbaya wa serikali ya CCM??
Je Mtanzania wa kawaida ,REGULA PIPO, ana mategemeo gani juu yamaisha yake mwenyewe??
This is a national security issue, just like a Cholera, TB or AIDS outbreak. We need to treat it with high importance.