Tanzanite ni Adimu kuliko Almasi; Tofauti ya Bei ni Promotion na Huenda Bei yake ikazidi kupaa

Tanzanite ni Adimu kuliko Almasi; Tofauti ya Bei ni Promotion na Huenda Bei yake ikazidi kupaa

Logikos

JF-Expert Member
Joined
Feb 26, 2014
Posts
15,460
Reaction score
24,233
Kuna mambo huwa nikawaza na kuwazua naona vitukuu watatushangaa Sana..., De Beers ameweza kupata pesa nyingi sana na kuwa Kampuni kubwa ambayo ni (Cartel) kwa kuweza kuwaaminisha watu kwamba Almasi ni Adimu sana na inapatikana kwa shida na sehemu chache sana (Ingawa ukweli Almasi ni nyingi ila wao ndio wanao-control soko) na wamewajengea watu fikra kwamba Diamonds are Forever na kwamba ni zawadi adhimu sana kumpa mpenzi wako mfano kwenye ndoa (yaani unamthamini zaidi)

Ila ukweli ni kwamba Tanzanite ni Adimu kiuhalisia na wala sio artificially kama Almasi, na inapatikana Tanzania tu (single source) na huenda miaka kadhaa ijayo kukawa hakuna tena Tanzanite ya kuchimba ingawa Almasi hata maabara unaweza kuzitengeneza na kuna watu wanazitengeneza....

Sasa cha kujiuliza kweli hili taifa letu ni la kuendelea kulalamika na wananchi wake kulialia njaa ? Ifike wakati kama taifa tuangalie jinsi ya kutatua matatizo yetu from within na sio kutafuta mchawi nje....

 
Hauijii vizuri almasi ww
Kwahio unadhani almasi ni Rare kuliko Tanzanite ?

Amini nakwambia Almasi imekuwa marketed kwamba ni rare kuliko ilivyo. Tanzanite inapatikana Tanzania pekee (Single Source) na Almasi ipo sehemu kibao na sehemu kama Mwadui ilikuwa unaokota tu kama Mawe same as South Africa; Kilichotokea De Beers na wengine wamezikusanya Diamonds za kufa mtu wanazo kwenye deposit hata leo wakiamua kushusha Bei ya Diamond hawashindwi; Kwahio kilichopelekea Diamond kuonekana Rare ni Supply is Controlled.
 
Back
Top Bottom