Hichi kifo cha mzee wetu mpendwa kitukumbushe kuwa hii dunia tunayoionea fahari si makazi yetu ya milele.
Hatuna budi kila mmoja wetu kwa imani yake kujiandaa na safari hii ngumu ambayo haakuna mtu anayeipenda wakati wowote na siku yoyote kwani hakuna ajuae ni lini atanyakuliwa kutoka hapa duniani.
Kwa wale wenzangu tunaoamini uwepo wa muumba na siku ya hukumu hatuna budi tujitathmini tutamtazama vipi muumba wetu kutokana na matendo machafu tuyatendayo hapa duniani?
Kama ungali unapumua wakati ndio huu wa kutubu dhambi zako na kuelekea katika ile njia iliyonyooka na impendezayo muumba.
Mungu amlaze anapostahili mzee wetu AMINI