TANZIA: Gwiji la utangazaji Ahmed Jongo afariki dunia

RIP Mzee wetu na mtangazaji bora ,Mzee jongo si ndie alitoa matokeo ya wao bila sisi moja mechi ya Simba na Yanga kati ya Timu hizo moja ilikua inaongoza yeye alikua mshabiki wa hiyo Timu...alisimamishwa kutangaza kabumbu kama alivyokua anaita mwenye...upande wa kaskazini na kusini wa Uwanja wa Taifa ...
 
Naongezea hapo

Omari Jongo

Dominic Chilambo

Charles Hilari

Walikuwa watangazaji bora kabisa wa mpira kwa wakati wote
 
Yy na omar jongo mtangazaji wa rtd zamani ndgu
 
Vipi wewe hauishi nchi hii na haujaja muda mrefu?
Majibu nitakayokupa ,hayatajibu swali nililo uliza ...Bado sijui kwanini ma Legendary wa Kitanzania wanakufa maskini ..nisaidie hapo tu
 
Thanks kuni tag, nilipo join RTD, Ahmed Jongo ndiye alinifanyia interview, na kwa vile mimi ngeli inapanda, nikapangiwa External Service.
RIP Ahmed Jongo.
P
Aisee! Ngoja niutafute uzi wako ule wa zamani unaohusu watanngazaji wa zamani RTD nione kama nitapata 2-3 za huyu mkongwe,nakumbuka kwenye uzi ule ulituhadithia hadi ulivyokoswakoswa na Ngoma huku wengine wakitoweka 1 by 1,hebu ngoja!
 
Utangazaji unalipa si unaona Kitenge anapata mpaka nauli ya kukwea Emirates Business Class kila wiki kuangalia EPL
Huyu marehemu alitangaza miaka ipi na Kitenge miaka ipi? Mishahara yao katika hizo radio au taasisi za serikali ni kiasi gani na pia mfumo wa mafao ya watumishi wa serikali baada ya kustaafu ina ukombozi wowote kwa mtumishi? Wachezaji wenyewe maarufu wa mpira wa miaka hiyo wengi wao wamekufa wakiwa na hali ngumu na hata ambao wako hai hali zao kimaisha zinasikitisha. Sasa kama wachezaji wenyewe hali zao ziko hivyo hali ya mtangazaji wa huo mpira unaochezwa na hao wachezaji si itakuwa ngumu zaidi?
 
RIP
 
Majibu nitakayokupa ,hayatajibu swali nililo uliza ...Bado sijui kwanini ma Legendary wa Kitanzania wanakufa maskini ..nisaidie hapo tu
Nimekuuliza hivyo nikimaanisha kwamba kwa mtanzania yeyote anaefuatilia mambo yanayoendelea nchini mwake hawezi kushindwa kujua kwa nini tunaowaita ma legend katika tasnia ya utangazaji na hasa hawa walio katika taasisi za serikali wanaishi katika maisha magumu kipindi cha utumishi wao na hata baada ya kustaafu. Ni sawa na kiongozi wa moja ya awamu zilizopita alivyodai kwamba hajui nikwa nini wananchi wake ni maskini! Uliwahi kujiuliza kuhusu mishahara yao katika hizo radio au taasisi za serikali ni kiasi gani na pia kama mfumo wa mafao ya watumishi wa serikali baada ya kustaafu ina ukombozi wowote kwa mtumishi? Wachezaji wenyewe maarufu wa mpira wa miaka hiyo wengi wao wamekufa wakiwa na hali ngumu na hata ambao wako hai hali zao kimaisha zinasikitisha. Sasa kama wachezaji wenyewe hali zao ziko hivyo hali ya mtangazaji wa huo mpira unaochezwa na hao wachezaji si itakuwa ngumu zaidi?
 
Thanks kuni tag, nilipo join RTD, Ahmed Jongo ndiye alinifanyia interview, na kwa vile mimi ngeli inapanda, nikapangiwa External Service.
RIP Ahmed Jongo.
P

Nawakumbuka sana weye na vijana wenzio wapya machachari mlokuwa mkiingia RTD.

Hivi weye na Abubakary Liongo si mlifuzu pamoja TSJ au weye ulikuwa wa kwanza pale RTD?
 
Naongezea hapo

Omari Jongo

Dominic Chilambo

Charles Hilari

Walikuwa watangazaji bora kabisa wa mpira kwa wakati wote

Marehemu Dominic Chilambo alifariki usiku baada ya kutangaza game ya Tukuyu vs Yanga, kina Seklojo Chambua wanaiua Yanga 2 - 1.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…