Mohamed Said
JF-Expert Member
- Nov 2, 2008
- 21,967
- 32,074
JOB LUSINDE (1930 – 2020) AFARIKI
Job Lusinde amefariki dunia leo tarehe 7 Julai siku ambayo mwaka wa 1954 wazalendo 17 walikutana katika ofisi ya TAA New Street, Dar es Salaam kuunda chama cha TANU kilichokuja kupigania uhuru wa Tanganyika.
Nilibahatika kukutana na Job Lusinde mara moja miaka kama miwili iliyopita tukiwa mazikoni Makaburi ya Kisutu na nikazungumza na yeye kwa uchache sana kiasi cha kumuomba nimpe kitabu cha Abdul Sykes na kumuomba kumpiga picha.
Aliyenifahamisha kwake alikuwa Saleh Tambwe na Mzee Lusinde alipokea kitabu changu kwa furaha.
Sijui kwa nini lakini Mzee Job Lusinde alinijia kama mtu mtaratibu kwa namna alivyokuwa anazungumza na mimi.
Nilimpa kitabu kwa kuwa nimemtaja katika historia ya TANU na uhuru wa Tanganyika yeye akiwa Dodoma wakati harakati za kudai uhuru zinaanza na alishuhudia kwa macho yake wakati wazalendo wa mji ule kikundi kidogo cha watu wakiongozwa na Omar Suleiman na Haruna Taratibu walipokuwa wakihangaika kufungua tawi la TANU pale mjini.
Job Lusinde kwa ajili ya kuhofia kazi yake akiwa mwalimu shule ya Alliance Secondary School alikuwa akifuatilia harakati zile kwa mbali na hakuwa peke yake waliokuwa na hofu hii ya kujihusisha na siasa.
Pale shuleni kulikuwa na kikundi cha wasomi kutoka Makerere, Lusinde akiwa mmoja wao ambao walitazama tu kwa macho yao na kusikiliza kwa masikio yao jinsi mambo yalivyokuwa yanakwenda Dodoma mjini.
Hawa wasomi wa Makerere hawakuthubutu kabisa kutia mguu katika harakati za kuunda TANU.
Jukumu hili la kuunda TANU waliwaachia fundi cherahani Omari Suleiman aliyekuwa akishona barazani kwake na Haruna Taratibu aliyekuwa fundi muashi Public Works Department (PWD).
Huenda historia mfano wa hii ndiyo iliyofanya historia ya TANU iogopwe kutafitiwa na kuandikwa kwani uhuru ulipokuja kupatikana mwaka wa 1961 wale ambao walijitolea kupambana na kila aina ya vitisho na madhila ya mpigania uhuru, kwa ajili ya kisomo chao kidogo siyo waliokuja kushika madaraka katika serikali ya Tanganyika huru.
Masharti ya Kura Tatu ya mwaka 1958 ya kuwa mgombea nafasi ya kuingia katika Baraza la Kutunga Sheria awe na kisomo cha darasa la 12 (baadae ikashushwa na kuwa darasa la 10) iliwatupa wazalendo hawa nje.
Waliopo madarakani wanaona fedheha kuwa wao juu ya elimu yao kubwa hawakuweza kuongoza mapambano dhidi ya ukoloni kazi hii wakawaachia wale ambao ukoloni ndiyo uliowanyima elimu na hata baada ya uhuru elimu ambayo waliitamani kuipata wakati wa ukoloni watoto wao hawakuipata katika Tanzania huru.
Kwa ajili hii basi historia ya kweli ya TANU na uhuru wa Tanganyika bado imekuwa kitendawili na wakati mwingine kuwaghadhibisha baadhi ya wasomaji wanaposoma majina na kuambiwa kuwa huyu alifanya lile na hili wakati wa kudai uhuru.
Mara nyingi huwa historia hiyo inayoeleza ni nzito lakini haijapata kusikika popote.
Bahati mbaya sana watu kama Mzee Job Lusinde walikuwapo wakati wa kupigania uhuru wa Tanganyika hawakushinda nafsi zao wakanyanyua kalamu kuandika historia hii.
Laiti wangeliandika ukweli ungelijulikana na wangeiachia nchi utajiri mkubwa wa historia ambao ungeishi kwa miaka mingi kama kielelezo cha mashujaa wazalendo waliopigania uhuru wa Tanganyika.
Picha ya nne kulia ni Haruna Taratibu, Saadan Abdu Kandoro, Julius Nyerere, Sheikh Mohamed Ramiya na Iddi Faiz Mafungo.