Ameugua bila msaada. Baada ya kufariki ndio tutaanza kuwaona viongozi wetu wakiwa kimbelembele kwenye mazishi na kumwaga sifa nyingi za kinafiki. ndio Tz yetu!
Dah,
Mungu anisamehe tu aisee, maana ni kama nlikua namchulia.
Huyu jamaa pamoja na mafanikio aliyoyapata kipindi anacheza, lakini ni mojawapo ya wachezaji wachache waliodumu kwenye game kwa muda mfupi sana.
Alicheza kwa kipindi kisichozidi miaka mitatu kisha akaachana na mpira huku akiwa katika kiwango cha juu. Wengi wetu tulidhani ni mtoto wa Mfanyabiashara Tajiri Bw. Alex Massawe hivyo tukafikiri kaamua kusimamia biashara za Baba yake.
Hivi karibuni aliekua mchezaji mwenzake timu ya Simba Boniface Pawassa (Baba Mwenye Nyumba) alidhamiria kuandaa mechi ya hisani kuchangisha hela za kumtibia Christopher lakini kutokana na urasimu mechi Mpaka leo haijafanyika.