Tanzia: Msanii Jebby afariki dunia kwao Dodoma

Tanzia: Msanii Jebby afariki dunia kwao Dodoma

"Angekuwepo rafiki nisingewaza,
Rafiki kipenzi niliyempenda,
Hayupo tena duniani SWAHIBA,
Nilompenda mpaka kumoyo SWAHIBA.

Alinisihi sana maisha haya, nisiwaseme watu kwa mabaya....."

My Mom used to love this song.

R.I.P Jebby, untill we meet again.
 
Msanii Jebby amefariki dunia leo akiwa nyumbani kwao Dodoma. Imeelezwa kwamba siku kadhaa zilizopita Jebby aliomba kurudi kwa Dodoma baada ya hali yake kuwa mbaya. Taarifa za awali zinasema alikuwa anasumbuliwa na uvimbe kwenye bandama.

Msanii Jebby atakumbukwa kwa wimbo wake wa 'Swahiba' aliomshirikisha Afande Sele. Wimbo huo umekuwa ukisikika kunapotokea msiba mkubwa na hata Masogange umauti ulipomkuta wimbo wa ''Swahiba'' umegongwa sana.

RIP Jebby.

Wimbo wa Swahiba

Hana picha ya passport size aliyopiga Bila swaga?
 
"Twendeni tukahani msibani vitambaa vyeupe mikononi x 2 yupo kwenye Jeneza Swaiba" Dah jamaa alikua na kipaji kikubwa sana ila Bahati hakuwanayo. Mfano nyimbo kama Swaiba, wanapagawa, Dunia haina siri, na hata kundi la Tmk alilolianzishi akiwa na Marehemu YP pia walifanya vizuri tu. RIP Jebby.
 
Duuuh sauti yake tu,so unique n huchoki isikiliza

Rest in peace Jebby
 
Back
Top Bottom