TANZIA Tanzia: Msanii wa kundi la Jagwa Music, Jack Simela afariki

Hua najiuliza sana hawa wanaoenda katika show za bongo flavour wanafuata nini hasa?
Binafsi sijawahi kuhudhuria lakini kupitia tv tuu sijawahi kuvutiwa kabisaaa.... ukijaribu kuangalia wenzetu ulaya live show zao utafurahi maana mtu hana playback
Mnanda unapigwa live huku unaona vyombo vyote na ubunifu, kule kwetu Yombo huu mziki una heshima yake
 
Piga keleeeeeeeeeeee oya dj dj ngoja kwanza dj stop kwanza
Oyaa mbona siwaskiia piga kelelee

Hah jamaa wananishangazaga sana
 
Hawa wana heshima zaidi ulaya ,bongo tunawaona wahuni, kidogo Sauti za Busara ndio huwa wanapanda ,hata baadhi ya nyimbo zao zina copyright ya nje

Mm nashangaaga watu wanajazana kumuona Diamond akiimba kwa playback wakati kuna watu wanapiga madude live kabisa cha kusitisha jamii haiwapi heshima wanayostahili
 
Miamba ya mnanda inazidi kutangulia mbele za haki.

Juma Mpogo keshakata kamba. Na sasa Jack Simela has joined the majority!! Daah R.I.P waswazi wenzetu.

From Temeke to Tandale, Tandika to Mbagala, Kigogo to Nyamala, Buguruni to Kiwalani... sote tunalia.

''Usiseme 'mpango mzima' mfukoni hauna hela''. by Simela. Long live mnanda.

Ladha za uswazi. Watoto mboga saba ushuani a.k.a Mom I need to Use your Car... hamuwezi kuelewa hizi ladha.

-Kaveli-
 
Dunia tunapita R.I.P Jack Simela

 
RIP Dogo Jack Simela, mmoja wa watu walinifanya nipende mchiriku.Poleni sana wapenzi wote Jagwa Musica.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…