TANZIA Tanzia: Msanii wa kundi la Jagwa Music, Jack Simela afariki

TANZIA Tanzia: Msanii wa kundi la Jagwa Music, Jack Simela afariki

Malumbano na zogo kubwa katika Basi lileeeee... Daah RIP Jack simela.
Kati ya kondakta na mwanamgambo yule, kondakta anadai nauliyakee eeh na mgambo anasema yeye ni chombo cha dola.

Bonge la song...Ila huu sio wimbo wa Jagwa ni kundi lingine nadhani.

 
Daah huu msiba mkubwa sana kwa sisi wapenzi wa muziki wa asili,wanangu wa kigogo,mburahati,manzese,mabibo mpaka mbagala.Alazwe pema mkali wa hizi kazi,sie bado tuko bampani.
Tabia na uzuri wake asha ukanifanya nikatoe barua asha daaah R.I.P simela watoto wa kiswaz ndio zetu mboga saba hawaziwez
 
Hawa jamaa ni hatari sana.
Asha
Oscar Mkoba
liwalo na liwe
Sarafina
Mwana wa Kitwana
Kichwa cha Nyoka
Kuluthumu
Mpangaji Mungu
Napenda sana hizo nyimbo.
Na ile Kondakta.
Nyimbo nzuri sana hizi aisee
 
Ukiwa wa 'mikoani' mchiriku huwezi kuuelewa!
Mchiriku ndiyo nini? Hilo neno 'Mchiriku' linatokana na jina la ndege Chiriku?
Mtu mwenye kubwabwaja au kuongea ongea mfululizo vitu visvyoeleweka tulikua tunamwita Chiriku, basi kama huo Muziki unaitwa Mchiriku utakuwa ni Muziki wa hovyohovyo sana hata ukaitwa Mchiriku.
 
Nimefurahiishwaa na kauli ya wazazii wanguu. Mimi dogo jakiii kwenda kuungana na jagwaaa....
Rip
 
Msanii maarufu wa kundi la Jagwa Music ambaye alikuwa nyota wa kundi kwa sauti yake tamu na Nzuri bwana Jack Simela ametutoka kwa ajali ya gari aliyoipata mkoani Morogoro kwa kugongana na Scania.

Hii ni pigo kwa mashabiki wa Mchiriku sio tu Tanzana bali duniani kwa ujumla sababu Jack Simela alikuwa na mashabiki wengi Copenhagen,Berlin,ulaya na hata Marekani kwakuwa Kundi la Jagwa Music mara nyingi walikuwa wanaitwa kufanya ziara kwenye nchi mbalimbali za barani Ulaya


-Saidi michape
-kondakta

Ni baadhi ya ngoma nazikimbuka za Jagwa Music ambazo Simela alizinogesha ..





View attachment 961310View attachment 961311View attachment 961312View attachment 961313View attachment 961314View attachment 961315

RIP
 
Back
Top Bottom