Tanzia: Msanii wa maigizo, Maureen Wana(Sabrina) afariki dunia

Tanzia: Msanii wa maigizo, Maureen Wana(Sabrina) afariki dunia

Replica

JF-Expert Member
Joined
Aug 28, 2017
Posts
1,681
Reaction score
8,887
TANZIA: Msanii maarufu wa maigizo Afrika Mashariki, Maureen Wana, ambaye pia alikuwa akijulikana kama Sabrina au Ketty katika tamthilia ya Kashfa iliyokuwa na Azam TV kupitia channel ya Azam TWO, amefariki dunia alfajiri ya leo.

Maureen amefariki katika hospitali ya Kilifi iliyoko mjini Mombasa kutokana na matatizo ya uzazi wakati akijifungua.

Msanii huyo atakumbukwa kutokana na umahiri wake katika uigizaji, uwezo wa kucheza nafasi mbili kwa wakati mmoja katika tamthilia moja.

Katika tamthilia ya Kashfa, Maureen alicheza ipasavyo nafasi ya Sabrina kama binti mshamba kutoka kijijini lakini pia aliweza kucheza vizuri kama Ketty, binti wa mjini na mrembo katika tamthilia hiyo hiyo.

Maureen ameacha mtoto mmoja wa kiume.

Azam TV tunaungana na familia ya Maureen, na wapenzi wote wa sanaa ya maigizo Afrika Mashariki kuomboleza msiba huu mkubwa.

 
Matatizo ya uzazi bado yanaua kina mama wengi sana nchi za kiafrika.

Hakika mwanamke kukubebea mimba ni sawa na kuweka maisha yake rehani, kwamba muda wowote anaweza kupoteza maisha.

Huku Afrika mimba ni sawa na hukumu ya kifo. Ni hatari sana. Lazima jitihada za maksudi zifanyike kuwanusuru dada zetu na vifo vinavyotokana na ujauzito.

Tima huu mwaka uanze nimeshuhudia watu wanne naowafaham kufariki kutokana na matatizo ya uzazi.

Poleni sana wafiwa. Ni wa wapi huyo dada, ndio mara yangu ha kwanza kumsikia.
 
hivi huyu si ni yule dada alikuwa anaigiza Kama mke wa yusuph mlela....daah apumzike kwa amani
 
sad,,kweli hii ni dunia ya 3..ujauzito unakua kama bomu la kujilipua
 
Back
Top Bottom