Tanzia: Msanii YP wa kundi la 'Wanaume TMK' afariki dunia

RIP YP.....tutaimiss ile flow yaki TMK .....
 
Msanii wa kundi la Wanaume Family "YP" amefariki Dunia jana usiku Hospitali ya TMK ambako alikuwa akisumbuliwa na kifua kwa muda mrefu lakini hali ilikuwa mbaya katika wiki mbili kabla ya kifo chake.

Meneja wa kundi la TMK Wanaume Family amedhibitisha kifo hicho na msiba hupo Keko nyumbani kwa baba yake.

Msanii YP aliimba nyimbo kadhaa kama Ulipenda Pesa', ‘Pumzika', ‘Shemsha' na nyimbo nyingi za TMK Wanaume Family kama ‘Twende zetu' ya Chege, ‘Dar mpaka Moro', ‘Kichwa kinauma',

Chanzo: Mtandao ya kijamii
 
Ebwana namsikiliza zembwela hapa kwenye supamix ndio amesema.

Yp ni msanii wa wanaume TMK aliyeimba kwenye dar mpaka moro akishilikiana na temba na chege au kwenye wimbo wa twenzetu akiwa na temba na chege.

Yeah alikuwa anapiga sana chorus pale Tmk wanaume nyuma ya chegge .....kibao kingine ni Pumzika (pale inapobidi)
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…