TANZIA: Mtoto wa Rose Nungu (Munalove) Patrick Peter Zacharia Komu (Partsmartboy) Afariki dunia

TANZIA: Mtoto wa Rose Nungu (Munalove) Patrick Peter Zacharia Komu (Partsmartboy) Afariki dunia

Uyo harlot mpaka mtoto azikwe atakuwa ka hit 1m followers, Everything is business nowdays
 
By Dk Levy


Ndiyo. Instagram ni eneo la wapuuzi. Siyo wapuuzi tu ni mchanganyiko wa mahayawani, wendawazimu, matutusa, mazuzu, mbumbumbu na wapumbavu wengi mno.

Kama kawaida jamii yetu ni ya mapokeo, tumepokea kila kitu. Bahati mbaya sisi wapokeaji tunaenda mbali zaidi na kuondoa kabisa maana ya vitu au kitu tulichokipokea. Tunavuka lengo la waanzilishi kwa kile tunacholetewa.

Familia zimesambaratika kisa mitandao, ndoa nyingi hazijafungwa kwa sababu hiyo. Watu wamefukuzwa au kuacha kazi kwa sababu ya upuuzi huu wa akili za kipuuzi.

Mitandao iko mingi, lakini instagram ndiyo kituo kikuu cha mambo yote kwa sasa. Huko ndiko akili mbovu zimeweka makazi ya kudumu. Na kila mtu kujiona yuko juu ya mwenzake.

Kila mtumiaji wa mtandao huu ni mwandishi wa habari. Ni mpiga picha mzuri. Ni mjuaji wa mambo ya watu na mwerevu wa kila jambo, na zaidi kila mtu mtakatifu.

Ukifanya kosa lolote likasambaa instagram, watu watakavyo kuongelea kwa lawama utaamini kuwa ni wewe pekee mwenye dhambi duniani na gari la peponi likija litakuacha.

Wiki hii kuna msiba umetikisa sana huko Instagram wa mtoto aitwaye Patrick, ambaye amefariki huko Nairobi alikopelekwa na mama yake kwa matibabu.

Mama wa mtoto anaitwa MunaLove. Ni wale wadada maarufu mitandaoni tu, kwa sababu ya muonekano wake, upambe (team) kwa mastaa wa mjini au kwa kile anachofanya huko mtandaoni.

Huyu umaarufu wake mitandaoni ni kwa sababu ya upambe wake kwa Wema Sepetu. Akawa maarufu na marehemu mtoto wake naye akawa maarufu kwa watu maarufu.

Kila kifo ni huzuni kwa mfiwa na jamii inayomzunguka. Hiki kimekuwa cha kuhuzunisha siyo kwa aina ya kifo au umri wa mtoto husika. Bali malumbano yanayoendelea kwa wazazi wake na jamii inayomzunguka.

Ni mambo ambayo neno sahihi la kuyatambulisha kwa watu ni ya kipuuzi. Ila upuuzi kauanzisha mama wa mtoto mwenyewe. Kwa kuamua kuweka maisha ya mwishoni mwa uhai wa Pati mitandaoni kana kwamba ni filamu mpya inatangazwa.

Kilichokera zaidi ni baba wa familia naye kuamua kuongea kila kitu kwenye vyombo vya habari. Huku mwili wa Pati ukiwa bado ndani ya jokofu kwenye moja ya vyumba ya kuhifadhia maiti pale Nairobi.

Ilitakiwa wawasiliane kama familia. Wafuate njia sahihi wafikie muafaka. Baada ya hapo achaguliwe mtu kama msemaji baada ya makubiliano ya kifamilia. Lakini wao mpaka Wema Sepetu na mama yake wakawa wasemaji.

Hawakumtendea haki mtoto. Haukuwa muda sahihi kuongelea matatizo yao huku mama wa marehemu hata baba yake wakijua fikra namna hivi sasa mitandao inakuza mambo. Kama ni kiki basi huu ni uzandiki.

Kila mtu anajifanya msemaji wa familia. Marafiki zake wanaongelea msiba kimamlaka. Wapumbavu wa kurasa za kipumbavu huko Instagram nao wanaongelea msiba kimamlaka. Watu hawaheshimu faragha za watu.

Miongoni mwa wajinga wa kurasa za kijinga huko insta walienda mbali zaidi kuwa mama anataka kujipatia pesa kupitia matatizo ya mtoto wake. Huyo mjinga naye ana wafuasi wengi wajinga wenzake. Ndipo unagundua kuwa Instagram ni sehemu ya kipuuzi mno.

Maajabu zaidi mama wa marehemu ghafla anapata nguvu. Anaandika waraka mrefu wa kuwasema watu wanamuongelea yeye vibaya. Kama hapendi kuongelewa vibaya aliyaleta mitandaoni kwa sababu gani?

Mbali ya kuandika waraka huo mreefu kuomba watu wavae viatu vyake kwa kipindi hiki. Pia nguvu za kusoma maandiko ya wajinga wa Instagram kazipata wapi katika wakati huu mgumu kwa mzazi wa kike kuondokewa na mtoto wake? Too much drama.

Kwa matatizo haya ya Munalove pia liwe somo endelevu kwa mastaa wengi wa sasa. Maana pamoja na matatizo mengi kuwatokaa wenzao lakini hawakomi. Acheni kuishi maisha ya kuigiza tazameni jamii inayowazunguka.

Leo upo na afya njema na nguvu ya kwenda kula bata zako. Ukifanya kitu cha kijinga na mashabiki kulaumu unawajibu nyodo na matusi juu. Keshokutwa yakikukuta unajisahaulisha na kuomba msaada wao. Badilikeni.

Mitandao ya kijamii kama instagram, imejipatia umaarufu mkubwa katika nchi za dunia ya tatu. Kutokana na tabia ya umbea na kuposti upuuzi kiasi cha kuwaharibia maisha bila wao kufahamu. Ama kupata madhara ya kisaikolojia ama hata kifo.

Kushuka kwa bei ya simu janja (Smart phones), na urahisi wa vifurushi hupelekea wengi kumiliki na kujiunga kwenye mitandao ya kijamii bila elimu sahihi ya malengo ya kuwepo kwake.

Hujikuta wakipost vitu ambavyo vinawafunua wao binafsi, jamaa zao na mataifa yao. Ni jambo la kawaida hivi sasa msichana kupiga picha ya utupu, na kutupia mitandaoni na akapata wafuasi wengi na yeye kuanza kuitwa staa baada ya miezi miwili.

Binafsi naamini matumizi bora ya mitandao ya kijamii ni kama kutangaza biashara au ujuzi wako ili uweze kufahamika na ikuletee tija. Badala ya kupiga picha ukila makange Kinondoni na kuandika ‘It’s happening now’.

Jamii yetu na utamaduni wa kutopenda kazi na kujikita kwenye umbea, lazima tutambue kuwa unapoweka kitu kwenye mtandao ina maana umeweka kila mtumiaji akione hata kama ni chako binafsi.

Kwa ujinga huu wa Instagram na kwenye mitandao mingi ya kijamii kama whatsApp.

Ningeomba serikali iongeze kodi za simu janja (smart phones), zisiwafikie watu wengi zaidi na kuendelea kuzalisha majitu mabwegebwege kupitia mitandaoni.

Pumzika Patrick. Mwendo umeumaliza ukiwa bado mbichi sana. Tupo nyuma yako.

Zaburi 27:10

Baba yangu na mama yangu wameniacha, bali Bwana atanikaribisha kwake
kwa hisani ya gazeti la Mwanachi

hivi instagram ndio sehemu gani, na ipo nchi gani vile!!!
Kama hayajakukuta ni rahisi sana kumponda Peter Kosovo kwa kuyaweka mambo sawa (to balance a story)...nimeanza kwa kusema, "kama hayajakukuta", hata hivyo nakubaliana na wewe juu ya ulimbukeni wa mitandaoni hasa kwa hao wanaotafuta kuonekana na umaarufu mchwara! Hii inatokana na kutojiamini wao wenyewe na hivyo 'approval' mitandaoni!...'attention seekers'!
R.I.P mtoto we Patrick!
 
hizi pumba zimeamia uku tena, bongo nyoso , bongo empty set kabisa, imekufa familia nzima mkuranga pale, hamna aliestuka, uyu mtoto mmoja ndio anatrendisha upuuzi huu kila kukicha!
 
hivi hizi dawa kwa watoto wadogo hazina madhara, huyu amepakwa madawa kichwani mda mrefu sana,
 
cc Mzigua90 ,hii imekaaje ?
FB_IMG_1531122112363.jpg
 
Back
Top Bottom