Kuna watu wamezaliwa miaka ya 2000 na kitu hawawezi kumjua uyo mama pia kunawemngine kipindi hicho walikua vjijini pasipokua na umeme hawakuweza kutazama mf; mie nilikua nasoma darasa la 5 wilaya ya tarime shule ya msingi Omuga, vijijini kabisa kipindi hicho sasa hv ni wilaya ya Rorya. ukiniambia maigizo ya RTD ya akina Onyango nitakuelewa japokua hao wa redioni wakifa hatuambiwi japokua walituelimisha tukiwa washamba kipindi hicho ndugu yako akitoka Dar majirani wanajua mnahela, ukimuona amekaa mahala hutaki kutoka hasa akiwa anapiga stori za Dar watu wanamsikiliza kila mtu anatamani arudi nae Dar, kipindi hicho anaongea baadhi ya watu wameishamuomba nguo alizovaa ili siku akiwa anarudi bongo awaachie, du! Watu tunatoka mbali siku nilipofika Dar ndipo nilijua kwamba, Dar watu waangaika kuliko mikoa mingine Tanzania hii, uuwii nimesahau hii THREAD ni ya msiba, Bwana alitwaa na Bwana ametua jina lake lihimidiwe.