Sheikh kazi unayo na pia usichoke, Mungu atakulipa kwa kutoa darsa bila khiyana. Usichoke, kadri dharau zinavyokuja, ndivyo Mwenyezi Mungu anakujaza majibu yenye hekima, busara na unyenyekevu wa hali ya juu. Hiyo ndiyo tofauti kubwa uliyonayo. Wengi wetu humu jukwaani tunajaa ghadhabu na pupa. Hapa sie wengine hupenda kusoma mada zako kwa kuwa pamoja na kuelimika lakini unatupatia darsa zuri la jinsi ya kukabiliana na ghadhabu, kejeli na dharau. Pia, wengine wetu hupenda kusoma na kufuatilia nyuzi zako ili tujifunze hicho ulichonacho, kinatoa mwanga mpevu. Hakika, Mungu aendelee kukupa umri na maarifa.