Tanzia: Mwanamuziki Geez Mabovu aaga dunia

Petro E. Mselewa

JF-Expert Member
Joined
Dec 27, 2012
Posts
10,307
Reaction score
25,932
GEEZ MABOVU AMEFARIKI DUNIA.


Msanii mkongwe wa muziki wa kizazi kipya hapa nchini Ahamedy Ally Upete aka Geez Mabovu amefariki dunia usiku wa saa mbili ya leo baada ya kusumbuliwa na maradhi kwa miezi kadhaa.

Wiki kadhaa zilizopita Geez Mabovu alielekea kwao Iringa kwa matibabu zaidi na ndipo hali yake ilibadilika na kuwa mbaya hadi umauti ulipomkuta hii Leo.

Chanzo: East Africa Radio
 


Taarifa zilizotufikia hivi punde zimedai kuwa rapper Geez Mabovu amefariki dunia leo mjini Iringa.

Kwa mujibu wa taarifa kutoka Iringa, Geez amefariki jioni hii.Alienda kwao wiki moja na nusu iliyopita ambako alianza kuugua mfululizo. Taarifa zaidi zinakuja.

December 27 mwaka jana, hitmaker huyo wa Mtoto wa Kiume alizidiwa ghafla kabla ya show iliyokuwa ifanyike mjini Iringa kwenye ukumbi wa Twista Night Club alikokuwa atumbuiza na rappers wengine wakiwemo Wakazi, Songa, Jan B na Chidi benz.

Chanzo:
Bongo5
 

Attachments

Mtoto wa kiume, mniache nijitume Kama matunda yangu yapo acha niyachume Nilishapita msoto tangu nilipokuwa shule Kama naungua na moto vile......

Kama ni kweli R.I.P mtoto wa mafinga dole south.
 
Reactions: m2u
Jamani nimeona kwa millard ayo rip mabovu kwani amekufa?
Nimeona mda si mrefu
mwenye uhakika atujuze maana jf ndo kila kitu!
 
Daah! Habari mbaya sana hii asee! Pole kwa wafiwa na wadau wa bongofleva kwa ujumla!

Nakumbuka baadhi ya nyimbo kama mtoto wa kiume na ile collabo ya wimbo wa 'mimi'

Jamaa alikuwa na kipaji na vocal kali sana! Sauti kali na kubwa kwa battle rhyms! Dah

Pole kwa clouds 'shem' wao wa zamani ndio katutoka!

R.I.P Geez Genious Mabovu!

Sent from my WhiteBerry using JamiiForums
 
Natamani kulia mwenzenu km nakuona vile

sauti ya zege daah
 
Kuna mchizi Jana alisema geez alikua anapiga viroba bila kula hadi figo zikafeli
 
Mimi zaidi ya msanii mimi kiooo cha jamii....R.I.P GEEZ MABOVU
 
Dogo asingejiunga na kundi la akina Langa na Babuu wa kitaa kula bange na unga na kutwa kushinda pale Container AAR alikuwa yuko fiti sana
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…