Mwanamuziki Moses Bushangama maarufu kama Mez B amefariki dunia. Mez B alikuwa mmoja wa Wanamziki wanaounda kundi la Chamber squard, amefariki leo mjini Dodoma.
Taarifa kutoka Dodoma zinasema kuwa msanii wa bongo fleva Mez B amefariki dunia muda huu. Alikuwa anaumwa sana homa ya mapafu, mama yake mzazi amethibitisha habari hizi za msiba akiwa Dodoma