Tanzia: Mwanzilishi na Bosi wa Tip Top Connection, Abdul Bonge afariki dunia

Tanzia: Mwanzilishi na Bosi wa Tip Top Connection, Abdul Bonge afariki dunia

ubarinolutu

JF-Expert Member
Joined
Oct 22, 2012
Posts
2,424
Reaction score
4,954
Kwa taarifa zilizotufikia ni kuwa bosi wa Tip Top Connection, Abdul Bonge ameaga dunia leo hii. Rip bonge.

attachment.php


Update:

Tasnia ya muziki wa kizazi kipya leo imepata pigo baada ya muasisi wa kundi la muziki la tiptop Abdul TaleTale (Abdul Bonge) kufariki jioni ya leo jumamosi

Abdul amefikwa na mauti alipokuwa akikimbizwa katika Hospitali ya Mwananyamala baada ya kusukumwa na kuanguka alipokuwa akiamulia ugomvi wa vijana karibu na nyumbani kwao Magomeni Kagera.

Marehemu atakumbukwa kwa kazi yake nzuri ya kuwaibua wasanii kama Madee, MBDog, PNC, PINGU NA DESO, KEYSHA, Z ANTON na Nk

Marehemu alipumzika kujishughulisha na Muziki na kumpisha Mdogo wake BABU TALLE Kuendelea na kazi hiyo.

Msiba upo nyumbani kwao Magomeni Kagera.
 
Bwana ametoa na Bwana ametwaa jina lake lihimidiwe

Taarifa zaidi zitakujia na kama kuna mtu anataarifa za ndani aweze kutujulisha

Source: clouds FM
 
Zisiwe tu za kweli jamani maana sasa hivi huu mtindo wa kuzusha hadi mtu unaogopa kusema R.I.P.
Kama ni kweli basi apumzike pema.
 
Kuna taarifa za kusikitisha juu ya kufariki kwa manager wa Tp top Connection . Mwenye ukweli atujuze
 
yeah amefariki... hata diamond ameposti hii kitu instagram

R.I.P Bonge
 
Zisiwe tu za kweli jamani maana sasa hivi huu mtindo wa kuzusha hadi mtu unaogopa kusema R.I.P.
Kama ni kweli basi apumzike pema.

Mwenzangu!social networks zimekuwa zinatumiwa isivyopaswa
 
Rip mjanja wa manzese,wote ni njia yetu wewe mbele sie nyuma.
 
Kazi yake mola haina makosa nadhani ndio wimbo ulomtambulisha madee kwa heri abdul bonge.
 
Back
Top Bottom