ubarinolutu
JF-Expert Member
- Oct 22, 2012
- 2,424
- 4,954
Kwa taarifa zilizotufikia ni kuwa bosi wa Tip Top Connection, Abdul Bonge ameaga dunia leo hii. Rip bonge.
Update:
Update:
Tasnia ya muziki wa kizazi kipya leo imepata pigo baada ya muasisi wa kundi la muziki la tiptop Abdul TaleTale (Abdul Bonge) kufariki jioni ya leo jumamosi
Abdul amefikwa na mauti alipokuwa akikimbizwa katika Hospitali ya Mwananyamala baada ya kusukumwa na kuanguka alipokuwa akiamulia ugomvi wa vijana karibu na nyumbani kwao Magomeni Kagera.
Marehemu atakumbukwa kwa kazi yake nzuri ya kuwaibua wasanii kama Madee, MBDog, PNC, PINGU NA DESO, KEYSHA, Z ANTON na Nk
Marehemu alipumzika kujishughulisha na Muziki na kumpisha Mdogo wake BABU TALLE Kuendelea na kazi hiyo.
Msiba upo nyumbani kwao Magomeni Kagera.
