Tanzia: Mzee Wangu, Wilinasi Mwendawila Sikanyika Amefariki Dunia na Kuzikwa (1951 - 2026)

Tanzia: Mzee Wangu, Wilinasi Mwendawila Sikanyika Amefariki Dunia na Kuzikwa (1951 - 2026)

Pole sana mkuu. Duniani tunapita ila inauma sana kupoteza mtu wa karibu.

Sasa ni zamu ya 1950-1959 kuachia nafasi duniani. Wa 40s ni kama wanaisha, wa 30s nadhani wapo wa kuokoteza sasa.
 
Pole sana kwa kuondokewa na huyu Baba yetu mzee Wilinasi. Tunaomba: Ee Mungu wa huruma na msamaha, tunaomba umjalie pumziko jema mtumishi wako Wilnasi, ukayatazame mema yake, na kumsamehe katika mapungufu yake, kwani alikutumainia wewe.
Ee Yesu Kristo uliyekubali kuuacha utukufu wako kwaajili ya wokovu wetu, tunaomba mateso na kifo chako msalabani visiwe bure, bali vikawe sadaka kamili kwaajili ya mtumishi wako Wilnasi. Wewe uliye mfalme wa faraja, ukawajalie faraja wanafamilia wa marehemu ili waupokee msiba huu kwa moyo wa unyenyekevu na matumaini. Bwana ametoa na Bwana ametwaa, Roho ya Wilnasi ipumzike kwa amani.
 
Amina. Asante sana mkuu kwa sala yenye kugusa moyo, maneno ya faraja na upendo. Katika kipindi hiki cha majonzi, maombi na faraja kutoka kwa watu wenye moyo wa upendo kama wewe ni sehemu ya nguvu inayotusaidia kuendelea kusimama. Tunamshukuru Mwenyezi Mungu kwa zawadi ya maisha ya Baba yetu na kwa muda aliotujalia kuwa naye. Tunaamini kwamba upendo na mema aliyotuachia yataendelea kuishi ndani yetu. Mwenyezi Mungu amjalie Baba yetu pumziko la milele, na akubariki sana kwa kutukumbuka katika sala zako.
 
Poleni sana.

"Hakika sisi ni wa Mwenyezi Mungu, na kwake Yeye ndiko tutakakorejea"
Hakika, sisi ni wa Mwenyezi Mungu na kwake tutarejea. Asante sana kwa kutukumbusha ukweli huu wa maisha na kwa kuungana nasi katika majonzi. Mwenyezi Mungu atujalie sote subira, hekima na mwisho mwema.
 
kwani hauna ndugu, jamaa na marafiki wa karibu wa kuwajulisha mpaka utangaze humu?

pole kwa kufiwa, rip ...
 
Amina. Asante sana mkuu kwa sala yenye kugusa moyo, maneno ya faraja na upendo. Katika kipindi hiki cha majonzi, maombi na faraja kutoka kwa watu wenye moyo wa upendo kama wewe ni sehemu ya nguvu inayotusaidia kuendelea kusimama. Tunamshukuru Mwenyezi Mungu kwa zawadi ya maisha ya Baba yetu na kwa muda aliotujalia kuwa naye. Tunaamini kwamba upendo na mema aliyotuachia yataendelea kuishi ndani yetu. Mwenyezi Mungu amjalie Baba yetu pumziko la milele, na akubariki sana kwa kutukumbuka katika sala zako.

Amina. Najua maumivu ya kuondokewa na mtu wa karibu kama Baba mzazi, Tunamwomba Mungu, hata katika magumu haya, wanafamilia mkazidi kusimama katika kweli ya Bwana. Tunamshukuru Mungu kwa nafasi aliyowajalia wanafamilia kupata nafasi ya kunufaika na upendo wa marehemu katika miasha yake, na upendo wake ukawe nguzo ya umoja, ushirikiano na upendo kati ya wanafamilia wote. Hatufahamiani katika mwili lakini sisi sote tu wamoja katika yeye aliyetuumba. Group letu linatunza siri ya itambuzi wetu. Naomba upatapo nafasi, niwekee namba yoyote au Lipa namba ambayo naweza kuweka chochote, naomba hicho nitakachoweka kikatumike kuomba misa takatifu kwaajili ya marehemu, aliyetutangulia kwenda kwa Mungu tunayemtumainia katika yote.
 
Pole sana mkuu. Duniani tunapita ila inauma sana kupoteza mtu wa karibu.

Sasa ni zamu ya 1950-1959 kuachia nafasi duniani. Wa 40s ni kama wanaisha, wa 30s nadhani wapo wa kuokoteza sasa.
30s kiasi wapo mkuu, 20s ndo wachache
 
Wana-JamiiForums,

Kwa masikitiko makubwa na majonzi mazito, ninawataarifu kuhusu kifo na mazishi ya mzee wangu mpendwa, Mzee Wilinasi Mwendawila Sikanyika, aliyefariki dunia tarehe 25 Oktoba 2026 katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Mbeya (iliyopo Wilaya ya Mbeya Mjini, Mkoa wa Mbeya) akiwa na umri wa miaka 75.

Mzee wetu amekuwa nguzo imara, kiongozi, na mfano wa kuigwa katika maisha yetu yote. Alizaliwa tarehe 12 Machi 1951 katika Kijiji cha Malolo, Wilaya ya Mbozi, Mkoa wa Songwe. Alikuwa mtoto wa pili katika familia ya watoto kumi na mmoja.

Mzee Sikanyika alikuwa mkulima wa kahawa na mfanyabiashara mwenye bidii sana. Alianza harakati zake za kibiashara mnamo mwaka 1979 katika Kijiji cha Hampangala, Wilaya ya Mbozi, Mkoa wa Songwe.

Baadaye alihamishia shughuli zake Kijiji cha Halambo, Wilaya ya Mbozi, Mkoa wa Songwe na kisha Kijiji cha Halungu, Wilaya ya Mbozi, Mkoa wa Songwe, kabla ya kurejea tena Kijiji cha Halambo mnamo mwaka 2000.

Kati ya mwaka 2007 na 2017, alihamishia makazi yake Wilaya ya Mbeya Mjini, Mkoa wa Mbeya, kabla ya kurudi tena makazi yake ya kudumu katika Kijiji cha Halambo, Wilaya ya Mbozi, Mkoa wa Songwe.

Katika maisha yake, mzee wetu alibarikiwa kuwa na wake watano. Ameacha jumla ya mke mmoja, watoto 18 na wajukuu 46 ambao kwa pamoja tunamlilia na kuenzi mchango wage mkubwa katika familia.

Mazishi ya mzee wetu yalifanyika rasmi tarehe 27 Oktoba 2026, ambapo mwili wake ulihifadhiwa kwenye makaburi ya ukoo yaliyopo Kijiji cha Halambo, Wilaya ya Mbozi, Mkoa wa Songwe. Familia tunatoa shukrani za dhati kwa ndugu, jamaa, na marafiki wote waliotufariji na kushirikiana nasi katika kipindi hiki kigumu.

Sisi kama familia tutamkumbuka daima kwa jinsi alivyotuhimiza na kutuunganisha katika umoja, ushirikiano, na upendo wa dhati. Tunakuaga kwa heshima kubwa, baba yetu mpendwa.

Bwana ametoa, na Bwana ametwaa; jina la Bwana lihimidiwe.
Pole sana kwa msiba huo mzito.
Bwana Ametoa, Bwana Ametwaa,Jina la Bwana lihimidiwe.
 
Back
Top Bottom