Hivi vitu viko wazi, kama vazi la kahaba,
Nasambaza maradhi, halafu nakupa Siku 7,
Machozi ni haba, Uokozi ni Njozi baba,
Ulimwengu wa Saba, Jehanam ya aina yake,
Kipe kitu kikupe, kikutupe kupe akikunyonya damu kwa hamu,
Kama hujafaham, DOGO mwanaharam,
Kalam inamwaga damu,
Nakuacha mweupe ka' mkorogo,
Chata ka' wagogo,
Wabongo acheni nyodo,
Wote mnakula hongo,
Hivi hii ni Serikali,
Au Sera Kali kwa mbali,
Au sera za mali,
Ni ipi, tafakari, nakufa kiume,
Tunapokwenda pana Zali,
Vichaa wangu walume wananyaka hiyo hali,
Tujitume, Pesa tuchume, kwa mwezi tudake,
Utake usitake, kila mjuba sasa kivyake mifuko itune,
Kama hujipendi njoo nichune, wabongo roho ziume,
Kama hufiki, usijikune,
Hivi inatiki,
Kila siku ya wiki,
Ikipata karatasi, wino hutoka kwa kasi,
Basi nina wasiwasi, kwa haya nawahasi,
Kiu ya Jicho, ulicho nacho ndicho ulicho,
Bongo ni Kama ficho, ya huwezi huchezi na anga,
Tokea '78 wabongo wamefunga mkanda!!