TANZIA: Producer Joshua Magawa "Pancho Latino" wa B hitz records afariki dunia

Kuna maeneo sio ya kwenda kabisa.
Nilivyokua nasoma comment kadhaa za watu nimepata idadi ya watu karibia kumi wamefia hapo! bado walioponea chupuchupu hapo. Hapo bado sjasoma comment zote.
Kwa kifupi mbudya sio sehemu salama watanzania tupate funzo hapa.
 
Toka rafiki yangu mmoja afe maji nishaamua kwa dhati kabisa kuwa nitakuwa naogelea sehemu za watoto na mabeki tatu.
Mnicheke msinicheki mtajijua wenyewe..
Ikifika siku yako hata maji ya ugoko yanaweza kukuuwa,hata glass ya maji iliyomwagwa chini,yanaweza kukutelezesha ukagonga kichwa chini chali,tunaanza kupitisha daftali la rambirambi,najaribu kukuonyesha kuwa kifo hakikwepeki,ikifika siku yako utakwenda tu,chafya inaweza kukuua,na ikikosekana sababu utafia hata usingizini,hapo hapo wavuvi wanakwenda baharini usiku kwa kutumia vyombo duni na wanarudi salama,unaskia mtu anamiaka 30 kwenye uvuv,au baharia anamiaka zaidi ya 20 anafanya kazi kwenye meli na anakuja kufa kwa maleria au uzee.
 
Hata mie imeniuma sana. Kuna beat moja ya Albino flani feat. Sugu &MwanaFA katisha sana. Acha hizi za Bado niponipo na Habari ndio hiyo. Dah. RIP Pancho!
Anaitwa Amani, mdogo wake Hermes.

Kwenye ile orodha ongeza:-
Mabeste,
Vanessa Mdee

Kaka ...
 
Naona wadau wanapalaumu Mbudya kwamba si sehemu salama paangaliwe bila kutoa onyo kwa wanaokwenda huko kujiangalia kwanza kabla ya kujitosa baharini kuogelea ikiwa ni pamoja ya wale mnaokwenda kama timu kushauriana maana watu wanakwenda ku-enjoy kule na wengine wanapiga kilevi pia (kuna uwezekano wwengine wamepata ajali kutokana na kuogelea huku wamepiga kilevi na kupepesuka majini ni kunywa maji kwa sana tofauti na nchi kavu ambapo utayumba utadondoka ukizidiwa watu wanakulaza pembeni kwa usalama ukizinduka unasepa na sio majini)..hivyo Mbundya ni salama kama ukiijua bahari ama ziwa huku ukifuata vigezo na masharti (patakuwa sio sehemu salama kama vifo vyote hivyo vinatokea kwa ajali za boat n.k)
 
Mbudya nilitaka kuzama mchanga wake wa bahari ndani ya maji mlaini ukikanyaga unatitia chini yani unazama na hayo maji ya kiuno tu na ubaya sijui kuogelea aliniokoa mtu mmoja tangu siku hiyo maji ya bahari siingii kabisa nakaa nchi kavu tu
RIP Mkaka
 
Toka rafiki yangu mmoja afe maji nishaamua kwa dhati kabisa kuwa nitakuwa naogelea sehemu za watoto na mabeki tatu.
Mnicheke msinicheki mtajijua wenyewe..
Hahahaaa umetisha upendo kwamba utakuwa unaogelea kwa watoto na Mabel Tatu we noma
 
Hahahaaa umetisha upendo kwamba utakuwa unaogelea kwa watoto na Mabel Tatu we noma
Maji sio mazuri kabisa,huwa naenda kwenye swimming pools kuangalia totoz tu huku nimekaa pembeni napiga vitu vyangu.
 
Mda nao ukifika..lazima binadamu aondoke...
Hizo nyingine ni sababu tu...
Ajali... na hata asingekwenda huko bado angeondoka kwa jengine!...

Wengine wanazaliwa..wengine wanakufa.. ...nature !
 
Huko mbudya kuna hotel? au kuna makazi ya watu? umeme upo?

Kitu kilicho nishinda ni maji yaani hunipandishi meli
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…