Tanzia: Sheikh Idd Nyundo afariki dunia

Tanzia: Sheikh Idd Nyundo afariki dunia

March 16, 2020
Zanzibar, Tanzania

Huzuni imetawala leo baada ya taarifa za kifo cha Sheikh Nyundo kilichotokea leo kutokana na presha. Marehemu Sheikh Nyundo amekuwa maarufu si mjini Zanzibar na Afrika Mashariki na Kati bali hata nchi za mbali kutokana kuwa maarufu kwa nasaha zake yaani daawa katika YouTube



Source : Ktv tz online
 
March 16, 2020
Mazishi ya Sheikh wetu mtu wa watu Sheikh Nyundo leo mjini Zanzibar Tanzania.

Sheikh Nyundo aliitumia teknolojia ya habari na mawasiliano vizuri kwa kutoa mawaidha ya kurekebisha tabia za wanajamii na mara nyingi kuwaacha wasikilizaji wakiangua kicheko kutokana na namna aliyoweza kuwakilisha ujumbe wake.

 
Mambo mambo yanapelekwa fasta fasta hivyo kulikoni?
 
Sheikh Nyundo alikuwa anajua kila kitu kinachoendelea mtaani au maskani na kuwa maarufu sana ktk vijiwe vyetu kutokana na kuongea yale yanayojiri ktk duniya hii yetu ya dotcom
 
Habarini za saa hizi?

Katika kuangalia status za Whatsapp naona watu wengi wame post Nyundo kafariki. Nimetafuta source sijafanikiwa. Najua humu ndio mama wa habari zote.Tafadhali tujuzane ni nini kimempata kama ni kweli.
Kama ni kweli nawapa pole ndugu zangu wanzanzibar na wafiwa wote.

Sheikh Nyundo ni Sheikh mwenye ushawishi mkubwa kwenye dini ya ndugu zetu waislam na amekua akikemea mengi mabaya waziwazi. Nadhani pia aliwahi kufungiwa kuzungumza kutokana na kuikosoa serikali ya Zanzibar mara kadhaa.

Sent using Jamii Forums mobile app

Unaonekana mchochezi....Hayo ya kuikosoa serikali unataka kurelate nakifo chake?


Sent from my iPhone using JamiiForums
 
Kutoka BAKITA, correct word ni marehemu. Neno 'hayati' linaelezea uhai. Hivyo huwezi kum-entitle mtu aliyekufa kama 'hayati'. Hao kamusi project nao wanachemsha.

Kwa maelezo zaidi wasiliana na BAKITA (Baraza la Kiswahili Tanzania).
Sahihi kabisa
 
Alikufa Tena 2009?
Kuna mkanganyiko hapa. Idd Nyundo aliyewahi wakati fulani kua Mkurugenzi wa Manispaa ndio aliyefunguliwa uzi mwanzo kabisa kua amefariki 2009.

Anayezungumziwa kufariki leo na kuzikwa ni Sheikh Hassan, maarufu kama Sheikh Nyundo. Idd Nyundo hakua Sheikh alikua mtumishi wa umma
 
Back
Top Bottom