RIP kada. TSN nini? MCT nini? Andika kwa kirefu
Sent using
Jamii Forums mobile app
TSN ni KAMPUNI ya Magazeti ya Serikali - Tanzania Standard Newspapers Limited
Tanzania Standard Newspapers Limited (TSN) ni shirika la umma lililoanzishwa tarehe 0 Februruari, 1970, chini ya Sheria ya Mashirika ya Umma, 1961. Hivi sasa TSN ni kampuni ya binafsi ya dhima yenye kikomo (LTD) inayomilikiwa na Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania yenye 99% ya hisa na Mhariri Mtendaji, ambaye pia ni Ofisa Mtendaji Mkuu wa masuuli (1% ya hisa).
Historia ya Tanzania Standard Newspapers Ltd imwanzia 1 Januari, 1930 wakati kampuni ya Kenya, East Africa Consolidated Holdings ilipoanzisha Tanganyika Standard Newspapers Ltd. Hata hivyo, baadaye kampuni ya biashara ya Uingereza, London-Rhodesia (LONRHO) ilinunua hisa nyingi Tanganyika Standard Newspapers Ltd mwaka 1961. Badala yake, iliunda kampuni mbili tofauti za Tanganyika Standard Newspapers Limited (TSN) na Printpack Tanganyika Limited (TPL). TSN ilichapisha Tanganyika Standard na Sunday News wakati Printpack iliyachapa. Mwaka 2006, TSN ilinunua mashine zake za uchapishaji.
Terehe 5 Februari, 1970, Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ilitaifisha Tanganyika Standard Newspaper na kuanzisha Tanzania Standard Newspapers Limited, shirika la umma linalomilikiwa na serikali.
TSN inamiliki na kuchapisha magazeti ya kila siku ya kurasa pana ya Daily News na toleo la Jumapili la Sunday News, Habari Leo la kiswahili ambalo ni dogo lilianzishwa mwaka 2006 na Spotileo, gazeti la michezo lililoanzishwa mwaka 2011. Aidha, inamiliki na kuchapisha magazeti matano. Katika kila wizara ya serikali, idara, mamlaka ya usimamizi na shirika, ni lazima wanunue na kusoma magazeti ya Daily News na Habari Leo.
Media Council of Tanzania(MCT) ni Baraza la Habari Tanzania. Ukitaka kuijua vizuri, muulize Kajubi Mwakajanga