Ndugu zangu,
january mwaka huu nilikuja hapa na habari za furaha kuu za kupata mtoto wa kiume (angalia link hiyo hapo chini)
https://www.jamiiforums.com/mahusia...a-kiume-mama-na-mtoto-wanaendelea-vizuri.html
leo hii nina huzuni kuu pia, Mwenyezi Mungu muweza wa yote kamuita mtoto huyo kurejea kwake na kutuacha na majonzi makubwa nisiyoweza kuyaeleza vyema. machozi mengi sana yamenitoka, ila sina la kufanya zaidi.
Bwana alitoa na Bwana ametwaa, jina la Bwana lihimidiwe
RIP mwanangu mpendwa
mpendwa Mtu Mmoja,
hapa duniani tunayo dhiki, tunajishibisha tu kwa "maganda ya nguruwe"!! lakini huko kwa Baba, hata watumishi wake wanakula na kusaza! (rejea kisa cha mwana mpotevu)
mimi najua kwa hakika huko kwetu (kwa Baba) NI PAZURI!!
wimbo:
KWETU PAZURI
kwaya:
AMBASSADORS OF CHRIST (kutoka Rwanda)
1.
ninayo hamu, kurudi nyumbani,
nyumbani kwetu ambapo hatutatengana
hapo nyumbani kwetu hakuna makaburi,
wala hakuna vyandarua maana hakuna marelia,
kwetu ni pazuuuri, ni pazuri nakuambia,
najua nawe ndugu yangu unayo hamu kufika huko
kiitikio
kwetu pazuri, nimeishapakumbuka
ninayo hamu kuishi na mwokozi wangu,
kwa amani na furaha tena ya ajabu,
sipati picha kwa watakaokufika kwetu mbinguni
2.
hii duniaa imejaa shida,
kama hujui, nenda hospitali kaone,
lakini kwetu hakuna fani ya tabibu,
watakatifu watachuma majani ya mti wa uzima
wawe na afya, hawataugua,
magonjwa tabu tutaziacha zote hapa duniani
kwetu pazuri....
3.
mpendwa njoo, turudi nyumbani,
asubuhi yaja tuyakimbie ya dunia,
atakayekosa kwa kweli ni hasara,
haya matatizo ni mitego ya shetani ili tushindwe
kufika nyumbani, kwetu pazuri,
lakini kwa jina jina la Yesu tumemshinda tunaenda!!
kwetu pazuri...
Bwana alitoa na Bwana ametwaa, Jina la Bwana libarikiwe
pole sana mpendwa na Mungu awazidishie imani katika kipindi hiki kigumu
msiache kuliitia jina la Bwana wa mabwana