Tapeli aliyekuwa anadanganya watu kuwa atawasaidia watu kupata ajira jeshini akamatwa

Tapeli aliyekuwa anadanganya watu kuwa atawasaidia watu kupata ajira jeshini akamatwa

Mindyou

JF-Expert Member
Joined
Sep 2, 2024
Posts
2,536
Reaction score
7,194
Jeshi la Polisi mkoani Singida linamshikilia mtu mmoja mwenye umri wa kati ya miaka 35 hadi 40 kwa tuhuma za kujifanya askari wa Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) na kutapeli mamilioni ya fedha kutoka kwa vijana wanaotafuta ajira jeshini, ambapo alinaswa Aprili 14, 2026 katika mtego uliowekwa na vyombo vya ulinzi na usalama

Alidai shilingi Milioni Moja kwa Kila Kijana​

Afisa mmoja wa JWTZ akizungumza na waandishi wa habari ameeleza kuwa walipata malalamiko kutoka kwa raia walioombwa kiasi cha shilingi milioni moja kila mmoja ili waweze kupata nafasi ya kujiunga na Jeshi la Kujenga Taifa (JKT).

"Zoezi la kujiunga na jeshi ni bure kabisa. Hakuna ada yoyote inayolipwa. Mtuhumiwa huyu amekuwa akipokea fedha na hata kuwaleta vijana kutoka maeneo ya mbali kama Itigi wakiwa na mabegi yao tayari kwenda jeshini, jambo ambalo ni utapeli wa wazi," alisema afisa huyo.

Walioathirika Wasimulia​

Mmoja wa vijana waliotapeliwa, Khalid Rajabu, amekiri kumpa mtuhumiwa huyo kiasi cha shilingi laki nne na nusu (450,000) kama malipo ya awali. Khalid ameeleza kuwa alikutana na mtuhumiwa huyo mjini Singida kupitia kwa mama mmoja ambaye alimtambulisha kuwa ni mtu mwenye uwezo wa kumuunganisha na jeshi.

 
Hao matapeli wanapata nguvu kwa sababu kuna watu wanaamini connection ndiyo kila kitu.

Ukiamini shortcut, lazima ukutane na watu wa aina hii waliopiga kambi Itigi kusubiri wenye akili fupi wazipeleke pesa zao kiholela.
 
Kumbe bado kuna watu wazima na vijana wajinga wanatapeliwa kirahisi hivi!
 
Hao matapeli wanapata nguvu kwa sababu kuna watu wanaamini connection ndiyo kila kitu.

Ukiamini shortcut, lazima ukutane na watu wa aina hii waliopiga kambi Itigi kusubiri wenye akili fupi wazipeleke pesa zao kiholela.
Hao wanaotapeliwa kwa namna hii miaka hii nao wakapimwe akili.
 
Nina uwakika ako na kadi ya fisiem ndio maana anajiamini kua yy n kada mtiifu kwao. Fisiem oyeeeeeeeh.
Kazi ni kipimo cha utu
 
Back
Top Bottom