Tararibu zipi za kufuata ili kuweza kusafirisha nyama nje ya nchi

Tararibu zipi za kufuata ili kuweza kusafirisha nyama nje ya nchi

Sir Kisesa

Member
Joined
Jan 30, 2020
Posts
25
Reaction score
23
Habari,
Kwa wazoefu wa Wanao safirisha Nyama Nje ya Nchi,
Nimepata soko tayari na nataka kusafirisha Nyama ya mbuzi nje,
Kuna mifuko ya package, nime attached ktk post naomba kujua naipata wapi, na kwa wazoefu zaidi wanipe utaratibu wote
Nishafatilia kibali board ya nyama, slaughter house nimeshafatilia.
Taratibu zingine za vibali kama zipo naomba kujua
FB_IMG_1738917117996.jpg
 
Mpaka hapo ulipofikia na information ulizopata Vibali n.k. zimeongeza kiasi gani cha gharama per Kg, kabla hatujaweka na mengine
 
Nyama ya ng'ombe China kilo inachezea Laki ..hili soko zuri sana ukipata fursa ya kuexport
Hizi habari umezitoa wapi mkuu ? Au ni Ng'ombe wa aina gani i.e. wamekidhi vigezo gani ?

 
Ahsante boss kwa sasa nimepata dubai nyama ya mbuzi, china tafatilia pia
Kwa soko la dubai kuwa nalo makini kidogo, nilisikia wamekataza kupokea nyama kutoka slaughtering house zingine yeyote TZ, isipokuwa 'kwa msomali- kibaha' na 'kuna mhindi yupo - arusha'. Fuatilia.

Na hawa wadau wawili hawaruhusu mtu mwingine kuchinjia kwao. Wanakwambia tupe huyo mteja wako tutampelekea sisi, Kama Cartel fulani wamejitengenezea, na wizara husika ipo kimya tu. Haya.

Kuna slaughering house ipo ruvu ndo wanasubiria vibali sina uhakika kama wameshapata, hawa waliruhusu watu wa kawaida kuchinjia kwao. Wacheck.

So jiridhishe kwanza na hizo taarifa usije fikisha mzigo ukawa rejected uka pata hasara.

Ila kama una updates mpya weka hapa ufaidishe na wengine. Maana mambo yanabadilika kila siku.
 
Mchi
Kwa soko la dubai kuwa nalo makini kidogo, nilisikia wamekataza kupokea nyama kutoka slaughtering house zingine yeyote TZ, isipokuwa 'kwa msomali- kibaha' na 'kuna mhindi yupo - arusha'. Fuatilia.

Na hawa wadau wawili hawaruhusu mtu mwingine kuchinjia kwao. Wanakwambia tupe huyo mteja wako tutampelekea sisi, Kama Cartel fulani wamejitengenezea, na wizara husika ipo kimya tu. Haya.

Kuna slaughering house ipo ruvu ndo wanasubiria vibali sina uhakika kama wameshapata, hawa waliruhusu watu wa kawaida kuchinjia kwao. Wacheck.

So jiridhishe kwanza na hizo taarifa usije fikisha mzigo ukawa rejected uka pata hasara.

Ila kama una updates mpya weka hapa ufaidishe na wengine. Maana mambo yanabadilika kila siku.
Vingunguti kuna baadhi ya vitu wanamlizia kufanyw registration ili warusiwe ku export Nyama.

Ukweli sector hii wakenya wanafanya sana kutokana nchi yao haina cost kubwa kama kwetu , tuna mzunguko mkubwa sana.
Fikiria
1. Unaanza kujisajili bodi ya nyama wana cost
2. Ukishasajiliwa wanakufanyia clearance napo cost nyingine
3. Wapime mfugo wakupe health certificate cost nyingine
4. Unatoka hapo unapeleka sample wizara ya kilimo wakupe permit napo cost
5. Unaenda posta kwa watu wa mionzi kupima nyama napo cost
6. Unaenda chamber of commerce wakupe certificate
7. Bado TRA

Alafu kibaya Taasisi zote hazipo sehem moja, dar unazunguka mpaka unajuta

Uko airport ndo wanaenda kukumalizia na price ya usafir.

Tanzania bado mazingira sio rafiki sana
 
Tarehe 1 Feb 2020
Uliomba kitabu cha mengi.

May 3 2024
ulikuja na fursa ya mafuta dumu 158 kwa faida ya 79,000.
500 profit ya kila dumu yakauzwe zanzibar. Ukaleta porojo ukamtaja mtu kaja inbox kwa na hakuwa amekuja akakuumbua.
Tena ulikuja kwa mantiki muwekeze na mtu milioni 10, ila kwenye maelezo ww ukajitoa huyo muwekezaji yeye ndie aje na m10, ww hatukujua faida yako nn.

Mara hamna transport cost, ni unaleta jamaa wananunua. Ikapita.

May 4 2024
Ukaja na uzi unasema kuhusu watu kujudge thread humu jf na kuzipa uhalali wa utapeli, ulikua unajitetea. Ukapata comment chache zilizokunganga.

July 6 2024
Ukaja na issue nyingi ya kutafuta aina ya chainsaw nzuri ya kukata mbao.

Sept 11 2024
Ukaja na kampuni yako ,ulisema una kampuni ya uuzaji wa korosho na avocado nchini.
Ikumbukwe huu huwa ndio mwisho wa msimu wa uuzaji korosho. Na hizi vitu vinaenda kwenye centres kwa mauzo ya jumuiya sio mikononi.
Ukasema kampuni yako ni mpya ukauliza unawezaje kupata wateja na masoko ya nje.
Mzee unafungua kampuni hujui unapata vipi tenda?

Sept 25 2024
Ukaja na kutafuta shipping company bongo wanaotoa bidhaa bongo kwenda dubai😂😂😂.
Yaani ukafanya kama ile china to bongo bussiness na bongo wapo. Hata research hujafanya, ukanangwa. Shipping au clearers na fowarders. Wengine wakasema nenda post wengine wakasema nenda EMS.

Jan 12 2025
Ukaja na uhitaji wa unga wa uwanga uliuita (arrow roots powder) ukamalizia kwenye mabano.
Ukasema unahitaji mwingi hata tani 5.
Akaja yukwapi. Akakwambia anayo tani 6. Ukamwambia akupigie simu. Ukapotea.

Februari 2 2025
Ukahoji kuhusu kama utafaidika ukifungua butcher la nyama ya mbuzi.
Na unataka kufungua Dar kwasababu umeona mabutcher mengi ni ya nyama ya ng'ombe. 🤣🤣🤣bucha la mbuzi dar daaah.

Ijumaa ya juzi hapa.

Ukaja na umepata soko la kusafirisha nyama ya mbuzi nje , soko lako liko dubai. Kuna aina ya mifuko ya packaging unahitaji.
Vibali bodi ya nyama na slaughter house ushafatilia. Meaning una slaughter house yako tayari.


Kuna kitu nimegundua. Unasikia sana story, unatamani kufanya vitu. Alafu pia unajitengenezea chembe za utaperi. Kila mtu anafikiria biashara ya kufanya. Ila wewe unakuja humu kiutaperi sana badirika.
 
Hii inchi tokea magufuri aondoke Duniani kila kitu mnauza nje,sasa sisi tutakula nini kama nyama mnauza nje yote?
 
Back
Top Bottom