Taratibu jamii ya Watanzania inaanza kuinyanyapaa elimu ya mtaala wa NECTA. Unaweza kuamini msomi kama Carol Ndosi anaweza kuandika kitu kama hiki

Ingekuwa instagram hii comment yako ningeipin mkuu umeongea bonge la point
Elimu yetu haitatui matatizo hata,wengi hata wa waalimu hasa wa msingi Wana akili ndogo Kama punje za
Kama huu ndio uhalisia mjanja ni nani? Ni yule anae tumia mamilioni kusomesha mtoto apate elimu ambayo haiwezi kumsaidia mtaani au yule mzazi ambae anamuacha mtoto wake kayumba kwa sababu anajua hata akilipa mamilioni haiwezi kuwa na mantiki yoyote
 
Yupo sahihi kabisa, Elimu ibadilishwe , ukikaa na watu wazima waliosoma miaka ya 80 kurudi nyuma utaona Elimu yao ilikuwa angalau bora kuliko ya sasa
Usisahau ndo wazee wetu walioko maofisini ndo maboss zetu tukipima uwezo wao tunaona hamna kitu elimu ya zamani watu walikua wana uwezo mkubwa wa kukariri sababu dunia haikua na mambo mengi kama sasa .

Mi nikiangalia hawa wazee wetu wengi napataga mashaka zaidi na elimu za zamani
 
Vilaza wanapata faraja sana kuona mtu aliyekua vizuri darasani kachapwa na maisha. Huu ndo Uchawi wenyewe

Kiuhalisia wengi wao wapo vizuri na wanaendelea vizuri na maisha yao. Wewe endelea kufundisha wanao wawe vilaza kama unapenda ukilaza.
 
Dah inasikirisha sana.
 
Bora wao kuliko sisi vijana 😂 wao walipata skills. Kuna shule moja juzi nimesikia inatangazwa redioni wanadai ukipeleka mtoto atafundishwa skills kama uchomeleaji, carpentry nk
 
Anayebeza elimu mi namwona mjinga tu unafikiri bila wataalamu nani atafanya kazi za ofisini tunahitaji wataalamu kama madaktari,walimu wa watoto wetu,ma IT, mechanics marubani nachoshauri serikali itengeneze mfumo wa watu bora kitaalumu wengine wawe katika daraja la kati kwa ajili ya operation na wengine wafanye ukasiriamali.

Tusisome kulenga tu kua matajiri ukiwa muaminifu tanzania kwenye ajira zetu sahau utajiri.
 
Kutofanikiwa au kufanikiwa kimaisha hakuwezi kuwa kipimo Cha msomi na asiyesoma!!, Mafanikio ya mtu inaweza kuchangiwa na wanaokuzunguka aidha umesoma au hujasoma na mtu mwenye akili timamu hawezi kushindanisha aliye na elimu na asiyo nayo.
 
Yupo sahihi kabisa, Elimu ibadilishwe , ukikaa na watu wazima waliosoma miaka ya 80 kurudi nyuma utaona Elimu yao ilikuwa angalau bora kuliko ya sasa
Tatizo ni elimu au tatizo ni maadili ya elimu?
 
Kama huu ndio uhalisia mjanja ni nani? Ni yule anae tumia mamilioni kusomesha mtoto apate elimu ambayo haiwezi kumsaidia mtaani au yule mzazi ambae anamuacha mtoto wake kayumba kwa sababu anajua hata akilipa mamilioni haiwezi kuwa na mantiki yoyote
Sema mimi nadhani ni namna tu ya ku mshape mtoto ajitambua akiwa na umri mdogo tu, maana kwa upande wangu tangu nifike kidato cha pili sijawahi kufatiliwa shule na mtu yeyote wala kuulizwa ripoti ya shule, na nimepiga tu st. Kayumba safiii, ila nilikua najua ninachohitaji labda background yangu ya maisha ilifanikiwa kunijengea attitude fulani ya kipambanaji
 
Elimu haipaswi kubezwa kama umetoboa kwingine na haukungoza darasani ni sehemu ya maisha tu. Hakuna cha kushangaza hasa kwa nchi kama Tanzania mtu anapata hela kwa uchawa anaishi kwa kuramba watu miguu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…