BASIASI
JF-Expert Member
- Sep 20, 2010
- 9,732
- 5,006
KUHUSU HILI LA DOLA TUKIENDA TARATIBU TUTAMUELEWA KATIBU MKUU
Magoiga SN
Katika nchi inayojiongoza kwa misingi ya kidemokrasia hususani demokrasia ya vyama vingi, Chama cha siasa kinapochaguliwa na wananchi kwa kura hupewa mamlaka ya kuunda serikali, serikali hiyo iliyoundwa inakuwa serikali yenye mamlaka na wajibu kwa watu wake walioichagua.
Kosa wanalofanya wengi wakisikia neno dola wanatengeneza tafsiri moja ya vyombo vya dola (Yaani vyombo vya ulinzi na usalama) UNAPOSEMA tuchagueni ili tushike dola tuwaletee maendeleo ni sawa na kusema, tuchagueni tushike serikali ili tuwaletee maendeleo. Vyombo vya dola vipo vingi sana siyo vya ulinzi na usalama pekee, hata mahakama ni chombo cha dola kinachotumika kutafsiri sheria na kutoa haki
Chama kilichoshika dola yaani chama kilichounda serikali kikiitumia dola vizuri kitafanikiwa ktk haya yafuatayo ;
i) Kitawaletea wananchi maendeleo ktk nyanja mbalimbali kwa kuunda wizara imara za kutekeleza mpango ya maendeleo na kuhakikisha uwepo wa fedha kugharimia miradi ya maendeleo,
ii) Kitadumisha ulinzi na usalama ndani ya nchi na kulinda mipaka yake kwa kuunda vyombo madhubuti vya ulinzi na usalama ,
iii) Kitahakikisha kila mtu anaheshimiwa utu wake kwa kujenga vyombo vya kutoa haki kama mahakama na mabaraza kuhakikisha kuwa kila mtu anapata haki yake
iv) Chama kitatumia dola , kuhakikisha huduma za jamii kama afya, elimu, miundombinu ya barabara na mengineyo yanawafikia wanachi ili kuwapunguzia kero ktk nyanja hizo nk nk. Fedha ambazo serikali ya CCM inatumia kujenga mahospitali, mashule, reli ya kisasa, madaraja nk ni mfano wa jinsi chama kinavyotumia dola/serikali ktk kuwahudumia wananchi na hivyo kujijengea jina na uaminifu wa kuchaguliwa tena
Kwahiyo chama kilichochaguliwa na kikaunda serikali kinakuwa kimepata jukwaa la kuwatumikia watanzania wote moja kwa moja ktk nyanja zote za kutatua changamoto zinazowakabili wananchi wake, kikifanikiwa kutatua matatizo kwa kiwango kinachoridhisha wananchi huweza tena kukichaguja chamma hicho hicho.
Kwahiyo chama kama CCM kina kitu cha kuwaonyesha watu kuwa nimefanya hiki na hiki na mkituchagua tena tutafanya hiki na hiki au kumalizia hiki na hiki maana ndicho chama kilichounda dola /serikali, lakini vyama vingine ambavyo havijawahi kuaminiwa na wananchi na kuruhusiwa kushika dola huwa wanajinadi kwa kusema mkitupa tutafanya lakini hawana cha kuonyesha kama mfano maana vyote vilivyopo vipo kwasababu ya chama kingine kilichounda serikali.
Bashiru hajasema atatumia jeshi la polisi au vyombo vya ulinzi na usalama kushinda uchaguzi.
Tatizo la Bashiru huwa akiongea hudhani kila anayeongea nae ana uelewa wa kuelewa alichokisema bila kufafanuliwa kwa lugha ya darasa la kwanza.
Naitwa Magoiga SN