Wasiliana na watu wa Masoko wa Kampuni za bia watakupa utaratibu. Kama uko mikoani kuna mawakala wakubwa (main distributors) wa makampuni hayo. Anzia hapo. Mahitaji muhimu kwa ufahamu wangu ni mtaji wa kutosha (sina uhakika na kiasi kwa kila kampuni), ghala madhubuti na gari. Mengine ni mambo ya leseni na kodi ambavyo havihusiani na makampuni ya bia moja kwa moja.
Asante sana kaka kwa mawazo yako huenda nikawa nimepata mahali pakuanzia lakini kwenye hilo swala la gari kwa mtaji nilionao kidogo ni ngumu lakini yale magali ya makampuni huwa hayatoi huduma hiyo?
mh kaka magari ya kampun ni kwa ajili ya kukuletea mzgo ila kama unataka kuwa AD (area distributor) unaingia mkataba na kampun then wanakupa mkopo thn unawalipa taratb kadri mtakavokubaliana na kama unataka kufungua store ya kawaida ambayo unaweza kuweka kama kreti 300 au 500 huhitaj gari tafuta hata guta tu kaka
JamiiForums uses cookies to help personalise content, tailor your experience and to keep you logged in if you register.
By continuing to use this site, you are consenting to our use of cookies.