Taratibu za kufuata ili kupata kibali cha kuendesha lodge

Taratibu za kufuata ili kupata kibali cha kuendesha lodge

Marahaba Mjukuu

Ili kujenga nyumba ya biashara (Lodge) kwanza ni lazima Kiwanja chako kiwe kimepimwa na kiwe kwenye upande wa Viwanja vya biashara ama Viwanja vya biashara na makazi n.k

Ni lazima uwe na kibali cha Ujenzi kutoka Halmashauri yako.

Kupata leseni ya biashara, unatakiwa uwe na TIN number pamoja na jina la hiyo biashara yako ambalo utaenda kulisajiri kwenye hiyo Halmashauri ambayo unaenda kuombea leseni.

Lakini ni lazima uwe na barua ya Mtaa/Kijiji (recommendation letter/introduction letter)

Pia utatakiwa kuwa na tax clearance form kutoka TRA

Ukishaomba utatakiwa kusubiri ndani ya Siku 7 hadi 14 hivi kuweza kupewa.

Jambo lingine la muhimu kabla hujaanza hiyo biashara hakikisha umepata ripoti ya ukaguzi kutoka Maafisa Afya/Mazingira/Kibali cha Zimamoto/Kibali cha OSHA n.k

Kila la heri kwenye Uwekezaji wa ndoto yako
Mtoa mada utakuwa umepata njia ya kuanza
 
Back
Top Bottom