Taratibu za kufungua Microfinance

Unashangaa hiyo boss
BOT kuna jamaa yangu ametaka kusajili biashara yake ni startup leseni bila kufanya chochote imegota 41M hii nchi ngumu sana na wanasema vijana mujiajiri
Ukiwaambia wasomi wanatuangusha wanakataa na kujitetea lakini wako busy kuhimiza vijana wajiajiri huku wakiweka startup environment ya kujiajiri kuwa ngumu sana. Mbaya zaidi, wala hawana mpango wa kubadilika. Haki ya Mungu, hatutoboi.
 
Hii nchi ngumu sana
Nimezunguka taasisi nyingi sana nchi hii kwa aina sheria zilizopitishwa na bunge letu ni ngumu sana kutoboa
 
Unashangaa hiyo boss
BOT kuna jamaa yangu ametaka kusajili biashara yake ni startup leseni bila kufanya chochote imegota 41M hii nchi ngumu sana na wanasema vijana mujiajiri
Hebu fafanua Mkuu, imegota 41 M, kivipi?
 
Hebu fafanua Mkuu, imegota 41 M, kivipi?
Payment system license 12M
Application fee yake ni 1M
Compliance za Payment system license unatakiwa uwe na approval ya TCRA na hiyo certificate kutoka TCRA application fee ni $1,000
Halafu liseni yenyewe ni $10,000
Hizo ni direct cost za compliance bado hujalipa consultancy wala Brela na wengineo
 
Unashangaa hiyo boss
BOT kuna jamaa yangu ametaka kusajili biashara yake ni startup leseni bila kufanya chochote imegota 41M hii nchi ngumu sana na wanasema vijana mujiajiri
Kuna biashara ni capital intensive na ukitaka kuifanta vyema lazima uwe na hela ya kutosha. Hii 41M nahisi itakuwa Internet Service Provider.

Kumbuka kuna infrastructure serikali iliweka kuwezesha ISP ifanye kazi kiufanisi. Sasa wewe unataka wakuwekee leseni 100,000. Hiyo hela watarudisha lini?? Na je taasisi itajiendesh a vipi?

Tatizo wengi hampendi kuchunguza kwanini vitu vipo hivyo vilivyo
 
Kama hawapendi kuchunguza iwaje wamefahamu hayo?

Issue ya kampuni kujiendesha inajibiwa na soko? Suala ni kuweka mazingira wezeshi kwa wazawa hasa vijana walau wakiweka 50% discounted itawawezesha sana na hata nia ya kuwasaidia itakuwa imeonekana. Maana mpaka mtu kuwaza hayo lazima na njia pia anakua amesha iandaa.

Sipendi kulalamika lakini hili ni suala la kutazamwa kwa jicho la ukaribu.

Kuna logic ya kuwasaidia kampuni za wazawa angalau tukue kwenye soko la ndani hapo hata akili ya kujitanua kwenye masoko mengine itakuwepo.

Kuminyana sana haina faida kwa mtu mmojamoja wala taifa
 
Kama hawapendi kuchunguza iwaje wamefahamu hayo?
Issue ya kampuni kujiendesha inajibiwa na soko? Suala ni kuweka mazingira wezeshi kwa wazawa hasa vijana walau wakiweka ...
Kuna sekta ngapi ambazo zipo wazi kabisa kwa wazawa ila hakuna tunachokifanya?

Tunapenda kulalamika sana ila sio kufanya jambo kwa ustadi wa hali ya juu.

Fursa zipo nyingi sana na kila kona ila tumelala doroo.

Kwa hiyo hata wangeweka 10 million bado kampuni nyingi zingekuwa ni wahindi, wachina, wajapan.

Tusipende kulalamika kwa kila jambo
 
Wakuu habari za sasa hivi...
Unapohitaji kuanzisha Microfinance na ili uweze kupata kibali cha kuendesha biashara yako kutoka BOT kitu cha kwanza cha msingi mtaji wako unatakiwa uanzie Tsh 20,000,000.
Vingine;
1. Ufanye usajili wa Kampuni au jina la biashara BRELA
2. Upate TIN na Tax Clearance
3. Uwe na Sera ya kukopeshea
4. Ada ya kibali ni Tsh 500,000 kea Kampuni na Tsh 300,000 kwa biashara binafsi.
N.k
Karibu sana kwa maelezo zaidi
Wasilana nasi kwa simu namba 0755 440 118
 
Hii 20,000M ni constant hata kama unafungua business name? Hata kama ni micro credit au microloan na si Microfinance ? Au ni kwa Microfinance pekeee hizi nyingine zina pungua capital yake
 
Hii 20,000M ni constant hata kama unafungua business name? Hata kama ni micro credit au microloan na si Microfinance ? Au ni kwa Microfinance pekeee hizi nyingine zina pungua capital yake
Ni constant mtaji ni huo 20m kwa sole proprieter, micro loan, microfinance au micro credit.
Ila kwenye hii biashara ni ndogo sana.
Ndogo mno.
 
Hakuna sababu ya kusema mtaji. Nakizi vigezo kwa mjibu wa kima cha chini.

Sajili jina la biashara BRELA.

Kisha nenda TRAujikadirie kodi japo watataka kukukadiria ila pambana iwe kodi rafiki.
Tengeneza file na uweke vifuatavyo.
1. Tax clearance ya madirector, na ya kampuni.
2. Bank statements za madirectors.
3.certified academic copies za directors,
4.CV za directors humu mnaweka na referres ili bank waweze kuwa contact.
5.Memorandum ya kampuni na lending policy.
6.Passport size photo za directors sikumbuki kama mbili au nne.
7.Vitambulisho vya madirectors.
8.Lipia maombi ya leseni kwa kutumia TISS sh 500,000.

Nenda BOT peleka watapitia.
Maombi ni mengi mno watapitia na watakurekebisha kidogo kidogo mpaka utafanikiwa.
Usichoke jamaa wanarekebisha kidogo kidogo mpaka mwisho utafanikiwa kupata leseni.

Ukipata karibu tupambane na wadeni wetu mtaani.
 
kwani hawa ndio wanaochukuaga kadi za benki za walimu?
 
I wish Mungu amuongoze jamaa akutumie wewe maana hatojuta
 
Laki 5 ni pesa ndogo kwenye usajili wa finance institute. Basically, I think if you're worried kupoteza 500k kwenye registration ya microfinance, maybe, just maybe you aren't ready for that business.
 
Laki 5 ni pesa ndogo kwenye usajili wa finance institute. Basically, I think if you're worried kupoteza 500k kwenye registration ya microfinance, maybe, just maybe you aren't ready for that business.
Kwani laki 5 ni kwa ajili ya nini? Kodi au ni kitu gani! Kama ni "kodi/levy" sawa ila kama ni 'administrative costs", that's relatively huge ili kuhamasisha microfinance.l,
 
Loan management system zinauzwaje boss?.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…