Taratibu za kumkataa msimamizi wa mirathi Mahakama ya mwanzo

Taratibu za kumkataa msimamizi wa mirathi Mahakama ya mwanzo

Joined
Aug 27, 2013
Posts
40
Reaction score
8
Heshimu kwenu wakuu nilikuwa nataka kujua taratibu zinazotumika kumkataa msimamizi wa mirathi Mahakama ya mwanzo jee unaandika ombi la kummkataa au unafanya vipi kwa sababu ni miaka miwili sasa tangu hukumu ya kumchagua kuwa msimamizi itoke na hajafanya chochote kuhusu mali za marehemu na nyingine zinazidi kupotea
 
....mh, utaratibu huwa ni kupeleka "ZUIO' (caveat) pia unaandika sababu za zuio mfano msimamizi huyo anatapanya mali za marehemu, pia mtu mwingine atatakiwa aombe usimamizi wa mirathi.
 
Asante mkuu pia nimejaribu kuwauliza watu wawili mmoja Hakimu na mwingine kutoka Chama cha wanasheria wanawake.Ambapo hakimu aliniambia naandika barua kwa hakimu aliyesikiliza kesi mwanzo ya kumuomba afanye mapitio hukumu yake kwa kumuelezea sababu za yeye kufanya mapitio hayo na yule kutoka Chama cha wanasheria akaniambia Nafungua kesi dhidi ya huyo msimamizi nikiwa na vithibitisho namna gani kashindwa kusimamia na aliniambia zuio tungeweza kufanya zuio kabla ya hukumu na si baada ya hukumu jee hapo unanishauri vp mkuu yupi kati yao yuko sahihi
 
Mkuu Mwanachondogoro ebu kwa uharaka soma article hiyo itakusaidia zaidi ukitaka maelezo niPM.

Ijue Sheria
[h=1]Sababu za kumuondoa msimamizi wa mirathi[/h]30/01/2014 | Posted by Kissima Adolf | Makala | 0 comments | 184 views |

LEO tutaangalia wajibu wa wasimamizi wa mirathi. Nitazungumzia juu ya usimamizi wa mirathi pamoja na mambo muhimu juu ya wanaonufaika na mirathi.
Katika Mahakama za Mwanzo pamoja na zile mahakama za juu kuna migogoro mingi inayohusu mirathi, kumpinga msimamizi wa mirathi au mashauri ambayo mara kwa mara hufunguliwa na ndugu wa marehemu wakimtuhumu msimamizi kufuja mali za marehemu.
Sheria ya usimamizi wa mirathi sura ya 352 ya sheria za Tanzania, ndiyo nitakayoirejea katika kuzungumzia wajibu wa wasimamizi wa mirathi.
Lengo kuu la sheria hii ni kutoa utaratibu wa kusimamia mali za marehemu baada ya kifo chake, ikiwamo kuhamisha umiliki wa mali hizo kutoka kwa marehemu kwenda kwa watu wenye haki ya kuzipata mali hizo.
Madhumuni hasa ni kwamba mali alizoacha marehemu zisibaki zikiharibika na kupotea bure, au warithi halali au watu wenye masilahi na mali za marehemu, mathalani wale wanaomdai hawapotezi haki hiyo, bali awepo mtu atayezisimamia na kuzigawa kwa wahusika wakiwamo wadai na kuepusha mgongano katika jamii husika.
Hivyo, sheria inamuweka msimamizi wa kugawa mirathi husika na mamlaka yake.
Kazi ya usimamizi wa mirathi ni kazi inayohitaji uaminifu wa hali ya juu.
Na ni vema ndugu wawe makini hasa katika kuchagua watu hawa kutokana na madaraka makubwa ambayo sheria inawapa.
Uchaguzi mbaya wa msimamizi wa mirathi unaweza kuleta madhara makubwa kwenye familia nyingi na matokeo yake mali hupotea.
Hebu tuangalie mamlaka ya kisheria aliyonayo msimamizi wa mirathi.
Msimamizi wa mirathi ndiye atakuwa mwakilishi halali wa kisheria wa mambo yote ya marehemu na mali zote za marehemu kisheria zitakuwa chini yake, na naomba ieleweke mali hizo zitakuwa chini yake kama msimamizi na si kwamba ni mali yake (si mmiliki).
Katika kesi ya Mohamed Hassan na Mayasa Mzee dhidi ya Mwanahawa Mzee [1994] T. LR 225 Mahakama ya Rufaa iliamua kwamba kisheria msimamizi wa mirathi halazimiki kupata ruhusa kutoka kwa warithi kabla ya kuuza mali yoyote ya marehemu.
Hata hivyo katika kesi nyingine ya Aziz Daudi Aziz dhidi ya Amin Ahmed Ally na Another CIV. App No.30 of 1990 [unreported] , Mahakama ya Rufaa iliamua kwamba pale tu msimamizi wa mirathi anapoteuliwa,mali zote zinakuwa chini ya mamlaka yake kama msimamizi na anachukua majukumu aliyokuwa nayo marehemu kwenye mali yake wakati yu hai.
Msimamizi huyu huachiwa kuamua jinsi ya kushughulikia mirathi hiyo kadiri atakavyoona inafaa.
Kwa upande mwingine, msimamizi atakuwa na mamlaka ya kufungua mashitaka mahakamani kwa niaba ya marehemu au kushitakiwa kwa niaba ya marehemu na atawajibika kulipa madeni ya marehemu kutoka katika mali alizoacha marehemu.
Msimamizi wa mirathi vilevile atakuwa na uwezo wa kuhamisha umiliki wa mali za marehemu kama atakavyoona inafaa kwa kuziweka rehani, kuziuza au kuzikodisha, kwa kuzingatia masilahi ya warithi na watu wanaomdai marehemu.
Hivyo ni sawa na kusema msimamizi wa mirathi hawezi tu kuamka na kutangaza kuuza mali za marehemu bila sababu za msingi.
Pia atawajibika kutumia kiasi fulani cha pesa za marehemu kwa ajili ya kutunza mali za marehemu ziwe katika hali nzuri na zisiharibike.
Msimamizi wa mirathi anatakiwa ndani ya miezi sita tangu apewe usimamizi au ndani ya muda mahakama ambao itaona unafaa, anatakiwa apeleke mahakamani na kuonyesha mali zote za marehemu na thamani yake halisi.
Madeni yake anayodaiwa au anayodai marehemu na ndani ya mwaka mmoja msimamizi wa mirathi atatakiwa tena kama mahakama itakavyoona inafaa, aonyeshe mali za marehemu zilizo mikononi mwake na jinsi alivyozifanya au kuzishughulikia.
Mahakama ina uwezo wa kuendelea kumuongezea muda mhusika kadiri itakavyoona inafaa.
Lakini kama msimamizi wa mirathi atatakiwa na mahakama kuonyesha mali za marehemu na akashindwa kufanya hivyo ndani ya muda aliopewa, atakuwa ametenda kosa la jinai na akipatikana na hatia atatakiwa alipe faini au apewe kifungo cha miezi sita.
Na kama ataonyesha mali hizo kwa nia ya kudanganya au kuficha atakuwa ametenda kosa la jinai ambalo kifungo chake ni miaka saba.
Mtu yeyote mwenye masilahi na mirathi anao uwezo wa kufanya ukaguzi ili kujiridhisha na usimamizi wa mirathi ya marehemu.
Msimamizi wa mirathi vilevile anatakiwa akusanye mali za marehemu na madeni aliyokuwa akidai na kulipa madeni aliyokuwa akidaiwa.
Katika madeni aliyokuwa anadai marehemu ni vizuri msimamizi wa mirathi akayadai mapema ili yasije yakapitwa na wakati kisheria.
Pamoja na hayo, msimamizi wa mirathi hatakiwi kujipatia faida kutokana na usimamizi wa mirathi hiyo na kama msimamizi wa mirathi mwenyewe au kwa kupitia kwa mtu mwingine atanunua mali ya marehemu, uuzaji huo unaweza kukataliwa kisheria na mtu yeyote mwenye masilahi na mirathi hiyo.
Moja ya sababu ya kufanya hivyo ni kwamba kuna uwezekano mkubwa akajiuzia mali hizo kwa bei ya chini kuliko thamani halisi ya mali husika.
Vilevile ni jukumu la msimamizi wa mirathi kutoa fedha kwa ajili ya shughuli za mazishi ya marehemu, ila gharama hizo ziangalie hali halisi ya maisha ya marehemu na kama ameacha kiasi cha mali cha kutosha kwa ajili ya shughuli hiyo; na kama msimamizi wa mirathi alitoa fedha yake kwa ajili hiyo, haki ya kwanza ni kulipwa fedha zake kabla ya madeni mengine ya marehemu.
 
....mh, utaratibu huwa ni kupeleka "ZUIO' (caveat) pia unaandika sababu za zuio mfano msimamizi huyo anatapanya mali za marehemu, pia mtu mwingine atatakiwa aombe usimamizi wa mirathi.
safi kwa jibu lako. nilikuwa najua ni hivyo pia.
 
Inaelekea kwa majibu yako haya unachokitaka kwa hatua hii siyo kumkataa Msimamizi wa Mirathi, ila nikupinga namna alivyo gawanya mali pamoja pia na hukumu ya Mahakama ya Mwanzo iliyokubaliana na ugawaji huo, ndiyo maana umeshauriwa juu ya Revision. Na wasiwasi unahitaji msaada zaidi.

255 654323268
 
mkuu shida yangu ni jinsi gani naweza kumtoa kusimamia na badala yake tumteue mwingine kwa sababu ni mzembe mno katika ufuatiliaji kiasi mali nyingine zinaelekea kupotea
 
Inaelekea kwa majibu yako haya unachokitaka kwa hatua hii siyo kumkataa Msimamizi wa Mirathi, ila nikupinga namna alivyo gawanya mali pamoja pia na hukumu ya Mahakama ya Mwanzo iliyokubaliana na ugawaji huo, ndiyo maana umeshauriwa juu ya Revision. Na wasiwasi unahitaji msaada zaidi.

255 654323268
Ikiwa ni hivyo unafanyaje mkuu
 
Ikiwa ni hivyo unafanyaje mkuu
...kama msimamizi alikuwa tayari ameshateuliwa, unatakiwa ufungue shauri dhidi ya msimamizi kuhusu utapanyaji wa mali za marehemu (huo anaofanya ni wizi kabisa) maana mali siyo zake.
 
Back
Top Bottom