Taratibu za kumshitaki mwajiri please

yahoo

JF-Expert Member
Joined
Sep 9, 2011
Posts
3,526
Reaction score
1,409
sijalipwa mshahara kwa muda wa miezi kumi,nimeacha kazi katika hiyo kampuni nikiwa bado nadi lakini mwajiri mbishi kulipa madai yangu akidai biashara ngumu ,naaminini si kweli) kwani kampuni bado ina exist kibiashara na amewaajiri ndugu kibao safu za juu huku ndugu hao wakizidi kununua magari.Nimeamua kumshitaki mwajiri-je nifate taratibu gani za kimahakama na pia nishitaki katika levo gani za kimahakama ili haki yanu ipatikane.MSAADA PLEAS:help:
 
Tafuta wakili hapo una madai km 300m wakili anachukua 10% tu wako wengi wanaganga njaa town wapelekee huo ulaji
 
Suala lako ni mgogoro wa kikazi ambapo masuala yote ya kikazi sehemu ya kupelekwa ni Tume ya Usuluhishi na Uamuzi au wanaita kwa kingereza Commision for Mediation and Arbitration kifupi "CMA", na njia ya kufikisha shauri hilo ni kwa kujaza fomu maalum ambayo inapatikana katika ofisi za vyama vya wafanyakazi au hata pale CMA au kwa mawakili.

Na migogoro imewekewa ukomo katika kufungua pale CMA na kama utakuwa nje ya muda uliowekwa kisheria itatakiwa upeleke kiapo(maombi) kuonyesha kwa nini umechelewa kupeleka au kufungua huo mgogoro katika muda uliowekwa na hiyo ipo ktk fomu namba 8 wanaita" application for late refferal of the dispute to the commission".

Migogoro iliyopo kisheria ni ya kihaki "Dispute of rights(huu mgogoro unatokana na vigezo na masharti yaliyopo ktk mkataba wa kazi) na wa kimaslahi dispute of interest(unatokana na mabadiliko ya hali ya kimaisha kwa tafsiri ya haraka kama vile mshahara wa mwaka 2007 hauwezi kukidhi mahitaji kwa mwaka 2012 hivyo wafanyakazi wakigoma kutaka kuongezea mshahara au hali bora ya maisha ndio aina hiyo ya mgogoro.

Kwa hiyo nikija katika suala la muda mgogoro unaotokana na kufukuzwa kazi "unfair termination"unatakiwa kuwasilishwa katika tume ndani ya siku thelathini (30) tangu ulipotokea na migogoro mingine inatakiwa kuwasilishwa ndani ya siku 60 na km utakuwa nje ya muda basi itatakiwa upeleka pamoja na maombi ukionyesha sababu za msingi kwa nini upo nje ya muda. Wakati wa ujazaji wa hizo fomu huwa zinatakiwa nakala tatu kwa maana moja ni ya tume(CMA), ya pili ya mwajiri na ya tatu ni kopi yako hivyo kabla ya kuzipeleka CMA.

unatakiwa umpeleke kwanza mwajiri wako aisaini ile nakala moja ya kurudisha CMA na nakala yake moja utamwachia na km itatokea amekataa kusaini basi utatakiwa kumtafuta mtendaji wa kata katika sehemu husika ambae utaenda nae hadi kwa mwajiri na akikataa kusaini mbele yake basi yule mwenyekiti atakuandikia barua kuwa ulipeleka ile fomu na mwajiri amekataa kuipokea atagonga na muhuri wake na utaipeleka CMA wataipokea na kutoa wito (summons) kwa ajili ya mwajili kufika ktk tume.

Kwamba utaratibu unaotumika ni kuwasuluhisha kwanza(mediation) na km ikishindikana basi mtaenda ktk hatua ya pili ambayo ni uamuzi(arbitration) ambapo hapo maamuzi yatakayotoka ni sawa kama ya mahakamani na km kuna ambaye hataridhika basi anaweza kuomba marejeo(revision) ktk mahakama kuu ya kazi.

Kwa kifupi ndio hivyo km kuna la zaidi wengine wataongeza.
 
Naomba msaada, Mimi nilifungua mgogoro CMA kwa kujaza form no1 na nikaainisha ktk form kwa kutiki makosa ambayo mwajiri alikuwa akinifanyia makosa yapatayo matatu ambayo yalinifanya niache Kazi kwa kulazimika, kosa la 1. Mwajiri alikataa kunilipa mshahara 2. Alianza kuninyanyasa baada yamimi kutoa vyeti vya ugonjwa ili nisiwe nafanya Kazi zaidi ya siku kuisha kwani alikuwa analazimisha mkimaliza kaz jion tuenderee kufanya masaa 2 zaidi mbere, lakini pia nililalamikia mwajiri kutokutekereza mashart ya mkataba, yote hayo niliyanot ktk form hiyohiyo, nanikajaza sehem ya partB , baada yahapo msuruhishi alibainisha kuwa mgogoro huo pa1 na mambo kuwa mengi utakuwa ni Termination , tulipoenda uamuzi muamuzi akasema form imekosewa kujazwa hivyo anashindwa kufream issue, japo hakukuwa na pingamizi upande wwte japo muamuzi alirekodi kuwa kunapingamizi upande wa pili nakunitaka nisaini jambo ambalo nililigomea kwakuwa hakukuwa na pingamizi, baadae akatoa uamuzi kuwa mgogoro umeletwa kimakosa hivyo baada ya kuwepo pingamizi hivyo anauondoa niupereke upya wakati mda wa siku 30 umeisha, naninajua nikipereka kwa maombi hataukubari maana mzungu amewaripa, Je Nifanyaje? Leo nisiku ya9 tangu uamuzi utoke nisaidieni.
 
pole sana ndugu yangu....hii ndio Tanzania ya viwanda...mkuu haki yako umepokonywa kama unaweza pambana hadi jasho lako la mwisho lakini itahitajika moyo wa ziada...maana kwa hicho walichokufanyia....ukijumlisha hali ngumu ya maisha mtu unajikuta unakata tamaa....Mwenyezi Mungu akuongoze katika kuipata haki yako
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…