Taratibu za kuomba mkopo wa Halmashauri (Mfuko wa Vijana)

hayolae

Senior Member
Joined
Sep 28, 2015
Posts
180
Reaction score
865
Wanajamii wenzangu, hongereni na poleni kwa mapambano dhidi ya COVID-19.

Niende kwenye maada moja kwa moja. Tupo vijana kama watano ambao ni wajasiriamali wadogowadogo tuna mpango wa kufuatilia na kuomba mkopo wa Halmashari-Fungu la Vijana.

Naombeni ushauri tufuate taratibu gani au tuwe na vigezo vipi ili tuweze kupata huo mkopo? Au nini tufanye ili tupate kwa urahisi huo mkopo?

Tunaomba mwongozo ili tutanapoanza kufuatilia basi tusipate vikwazo vingi.

Natanguliza shukrani.
 
1. Inatakiwa msajili kikundi chenu kwa afisa maendeleo wa wilaya yenu.

2. Inatakiwa mfungue akaunti benki ambayo itatumika kuingiza mkopo wenu.

3. Mnatakiwa kuwa na kiasi cha fedha kwenye akaunti yenu kama elfu thelethini tu.
Mengine utayapata ukienda kwenye ofisi za maendeleo ya jamii.
 
Ahsante sana mkuu. Nipazima pia muwe na mradi unaoendelea wa kikundi??

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Utaratibu wa sasa vikundi vya vijana na vile vya wanawake 10-15.Ila vya walemavu ni 5.Pia ukisajili kikundi sio lazima kupewa mkopo ila wataangalia shughuli wanazozifanya hao wanakikundi zinaleta tija ili mukipewa pesa irudi.NB pesa haina riba
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…